Arteta: Mechi 3 Kuamua Msimu Huu.

Kocha wa Arsenal – Mikel Arteta ameweka wazi kuwa wiki ijayo itaamua hatma ya kikosi hicho kwa msimu huu.

Arsenal wapo katika hali mbaya kwenye EPL msimu huu wakiwa wameshinda mchezo 1 kati ya 10 iliyopita na wanashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa EPL.

Arteta atakuwa mwenyeji wa Frank Lampard wakati Arsenal itakapowakaribisha Chelsea leo usiku. Baada ya mchezo huu, Arsenal watachuana na Brighton pamoja na West Brom. Hizi ni timu 2 zilizopochini ya Arsenal kwenye msimamo wa EPL.

Bila kupindisha maneno, Mikel Arteta amesema “Sina visingizio. Siku 7 au 8 zijazo zitakuwa za muhimu, zitatuonesha ni wapi tunaelekea kwenye Premier League.

“Nimekuwa muwazi tangu mwanzo kwamba tunapoteza michezo. Ni jukumu langu kusuluhisha hilo, bila kujali kitu chochote ni sisi tunaojianguasha wenyewe na ni sisi tunaopaswa kubadili hilo.”

Siku ya Jumatano, kocha wa West Brom – Sam Allardyce aliwataja Arsenal kama timu wanayoshindana nayo kwenye nafasi za kushuka daraja msimu huu. Kwamba haoni tofauti ya timu yake na Arsenal.

Kuelekea kwenye mchezo huu, Frank Lampard aliwaumiza Arsenal hapohapo Emirate msimu uliopita na Chelsea wamepoteza mchezo 1 pekee kati ya 9 waliyocheza dhidi ya Arsenal.

Hali itakuaje leo usiku. Ni Arteta au Lampard kuendelea alipoishia?


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

12 Komentara

    Hapa arteta inabidi ajitahidi sana la sivyo atashika mkia

    Jibu

    Jamani hadi huruma aongeze juhudi atashinda

    Jibu

    Dar anatakiwa aongeze juhudi atapata ushindi

    Jibu

    Daa Arteta anakazi kubwa sana

    Jibu

    December siku zote inakuwa ngumu kwa Arsenal alkini msimu huu Arteta amekaa pabaya sana

    Jibu

    Duuh arteta ana kazi kubwa Sana.

    Jibu

    Waongeze juhudi

    Jibu

    Arteta ajipe kipind

    Jibu

    Wapambane

    Jibu

    Arteta wajipange wapambane ili waweze kupata ushindi

    Jibu

    Jamanii

    Jibu

    Wajipange upyaaa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.