Azam FC Yaondoshwa Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Klabu ya Azam Fc ambayo makao makuu yake yapo Chamazi imeondolewa kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa kwa Agg ya (3-2) na timu ya Al Akhadar na timu hiyo ya Libya kusonga mbele.

 

Azam FC Yaondoshwa Michuano ya Kombe la Shirikisho

Mechi ya kwanza wakiwa ugenini Azam walifungwa mabao 3-0 bila hata kupata bao lolote kitu ambacho kilifanya mlima kuwa mkubwa wa kupindua meza na timu hiyo ya Libya ilionekana kutaka matokeo wakiwa nyumbani kwao.

Mechi ya marudiano ya hapo jana wanalambalamba hao walicheza kwa hali na mali ili kutaka kupindua meza kama ingewezekana huku kumalizika dakika 45 za kwanza wanalambalamba walikuwa wanaongoza bao 1-0 huku wakikosa nafasi za wazi kadhaa.

Kurejea kipindi cha pili walikazana kushambulia lango la mpinzani huku wageni hao wakionekana kuwa hawakuhitaji sana kutumia nguvu ya ziada kutokana na mtaji wa mabao waliyokuwa nayo.

Azam FC Yaondoshwa Michuano ya Kombe la Shirikisho

Dakika ya 58 yuleyule Idris Mbombo anapachika bao lingine la pili na kufanya ubao usomeke 2-0, kutokana na kukosa ufanisi mpira unamalizika kwa mabao hayo hayo mawili na kufanya timu hiyo kutolewa kwenye michuano hiyo baada ya aliyekuwa akishiriki pia michuano hii Geita Gold kuondolewa.

Kwahiyo mpaka sasa timu mbili kutoka Tanzania zimeondolewa kwenye michuano hii ya Kombe la Shirikisho barani Afrika Azam pamoja na Geita Gold.

 

Acha ujumbe