Baada ya Liverpool kuwalaza na viatu wageni wao wa mchezo wa jana, Spurs bado kuna ugumu kuelekea nani anaweza kutwaa ubingwa wa ligi hiyo baada ya matokeo ya mechi hiyo ya jana. Tottenham walionekana kutokuwa na bahati katika mchezo wao huo kutokana na kutawala sana lakini wakashindwa kabisa kupata matokeo yaliyotakiwa.
Yalikuwa ni makosa ya mlinda mlango na mlinzi namba moja wa kikosi hicho, Hugo Lloris ambaye alishindwa kuzuia ipasavyo mipira iliyokuja upande wake hata ile iliyokuwa na uwezo wa kuikamata bila kuathiri mashambulizi ya wachezaji wengine. Kwa lililotokea anastahili kujifikiria na kutathmini juu ya mapungufu hayo yaliyotokea upande wake.
Spurs walionekana moto kwenye mechi hiyo baada ya Lucas Moura kuwarudisha mchezoni kwa kusawazisha goli lililowekwa nyavuni na Firmino katika kipindi cha kwanza. Baada ya hapo wakafanikiwa kuutawala mchezo kwa asilimia nyingi jambo ambalo lilionekana kabisa walikuwa na nia ya kupata ushindi kwenye mechi hiyo.
Lakini dakika za mwisho kabisa za mchezo Hugo alifanya makosa yaliyowagharimu kwa kushindwa kuudaka mpira rahisi wa kichwa uliopigwa na Salah na kujikuta akiutema mpira huo moja kwa moja na kumkuta mchezaji mwenzake Toby jambo lililopelekea kufunga goli la uzembe kabisa dakika za mwisho za mchezo.
Nyota huyo wa Ufaransa amekubali kabisa kuchukua lawama zote kwenye mchezo huo baada ya kushindwa kuzuia mpira huo na kusababisha kosa lake kuigharimu timu yake. Kuna wakati vitu vya namna hiyo huonekana ni vya kawaida na vidogo lakini kwa upande mwingine huweza kugharimu timu kupoteza kabisa alama kwenye mechi zake.
Pamoja na makosa hayo na matokeo ambayo wengi yaliwasikitisha lakini mwalimu wa kikosi hicho, Pochettino aliyeshuhudia mechi hiyo akiwa sehemu ya mashabiki nje na eneo lililozoeleka kwa makocha kuwepo amewasifia wachezaji wake kwamba hata kwa hatua hiyo wao ni wapambanaji na wanastahili pongezi kwa makubwa waliyoyafanya kwenye mchezo huo.
Walipata nafasi katika kipindi chao cha pili lakini bahati haikulala upande wao wakajikuta wanashindwa kuitumia pale Sissoko aliposhindwa kufunga mpira wa wazi kabisa kati yake na golikipa huku wakiwa wamefanikiwa kumtoka mlinzi wa timu hiyo. Huenda wangeutumia mpira ule mambo yangekuwa tofauti kwao.
Kwa ushindi huo sasa, Liverpool anarejea kileleni akiwa na michezo yake 32 na alama 79, huku mpinzani wake Manchester City akiwa nafasi ya pili kwa nyuma ya mchezo mmoja [31] na alama 77 ambapo matokeo ya mchezo huo ambao ni kama kiporo utaamua nani anayestahili kukaa kwenye kilele cha ligi hiyo au kushuka nafasi ya pili. Japo kiporo cha Man City bado ni kigumu sana.


Povel
Gud news