Yaliyojiri PL

Manchester United wameanza kampeni yao vizuri ndani ya ligi yao baada ya kupata ushindi mbele ya Watford ambao walijitahidi kutawala mchezo japo bahati haikuwa kwao. Ushindi huo ni wa kwanza kwa Ole Gunnar Solskjaer akiwa kama kocha wa kudumu wa klabu hiyo baada ya kupewa kandarasi ya kukifundisha kikosi hicho kwa miaka mitatu.

United walipata uongozi dakika ya 28 tu ya mchezo baada ya walinzi wa Watford kupandisha mashambulizi na kujisahau kurudi kuzuia ndipo Rashford alipotumia mwanya huo kwa kupigiwa mpira wa haraka uliowapa ushindi huo United katika dakika za mapema kabisa za mchezo; ikiwa ni pasi murua kabisa kutoka kwa Luke Shaw.

Hadi kipindi cha kwanza kinaisha United walikuwa mbele kwa goli moja pamoja na kucheza soka ambalo halikuwa na mvuto sana ikiwa sio kawaida kwa timu hiyo. Kwa namna nyingine tunaweza kusema bahati ilikuwa upande wao katika mechi hiyo kutokana na soka safi walilolionesha Watford.

Katika kipindi cha pili, Watford waliendeleza harakati za kutafuta goli la kusawazisha huku wakilisakama lango la United mara kwa mara lakini wakakosa umakini wa namna ya kuwaadhibu kwa namna walivyopata nafasi nyingi za kuzitumia. Hii inakumbusha ule msemo wa mtoto halali na pesa.

Kutokana na kipindi cha pili kuanza tena kuwa nje ya matarajio yao, United wakapata goli dakika ya 73 kupitia kwa Antony Martial aliyefunga goli lililokuwa gumu sana baada ya mpira kumtoka mlinda mlango Foster aliyeshindwa kuukamata kwa ufundi wa pekee na nyota huyo raia wa Ufaransa.

Pamoja na kuwa nyuma kwa magoli hayo mawili; Watford hawakuweza kukubali kirahisi waliendeleza kasi ya mashambulizi kama kawaida kuelekea kwenye lango la mpinzani wao na hii iliwasaidia kwani dakika ya 90 ya mchezo waliweza kupata goli la kufutia machozi kupitia kwa Abdoulaye Doucoure aliyefanya kazi kubwa sana kwenye mchezo huo.

Ushindi wao wa 2-1 ni hatua nzuri kwao wakiwa kwa sasa wamerudi nafasi ya nne kwa muda wakisubiri Arsenal acheze mechi yake. Na katika nafasi hiyo wanazidi kuombeana mabaya yaweze kumtokea ili wapate nafasi ya kuendelea kukaa kwenye nafasi hiyo. Kupitia hilo nafasi inazidi kuwa na mvuto wa kiushindani baina ya klabu hizi tatu.

Man of the match

Katika mechi hiyo Rashford anabaki kuwa nyota wa mchezo baada ya kufanya kazi kubwa na ya pekee ndani ya mchezo huo akiendeleza matokeo yake safi kwa mechi anazopangwa; huku upande wa pili kukiwa na raia wa Ufaransa aliyeweza kulitumia dimba vizuri, Abdoulaye Doucoure akiwa amefanya kazi kubwa sana na ya pekee kwenye mtanange huo.

Yajayo

Baada ya ushindi huo United anajiandaa kumkabili Wolves katikati ya wiki na Watford watakuwa wenyeji watakabiliana na Fulham.

Makala ijayo

2 Komentara

    Safi

    Jibu

    Ligi safi

    Jibu

Acha ujumbe