Barca Wanamkumbusha Dembele Kuondoka.

Wakati zikiwa zimesalia siku 4 dirisha dogo la usajili, Barca wanamkumbusha Ousmane Dembele kuondoka klabuni hapo.

Barca wamechoka kubembeleza wachezaji linapokuja suala la mikataba. Wakati huu ambao timu inataabika kiuchumi, Barcelona wanajitahidi kupunguza matumizi ya uendeshaji wa timu hiyo ili kuendana na sheria na kanuni za kifedha za LaLiga.

Wachezaji nyota kama vile Pique, Alba na Umtiti, wamepunguziwa mishahara maradufu ili kuendelea kubaki Camp Nou. Hali haipo hivyo kwa Dembele.

Mchezaji huyo amebakiza miezi kadhaa mkataba wake kuisha mwishoni mwa msimu huu. Amegoma kusaini mkataba mpya aliopewa na Barcelona na, baada ya muda mrefu wa majadiliano yasiyofikia suluhisho, klabu imeamua kumfungulia milango mchezaji huyo aondoke Camp Nou ndani ya siku 4 zilizobaki.

Japokuwa Dembele anataka kubaki klabuni hapo walau mpaka mwisho wa mkataba wake, uongozi wa klabu hautaki hilo litokee, wanamtaka Dembele aondoke sasa hivi na kama akishindwa kupata timu, Barcelona wenyewe wapo tayari kumsaidia kupata timu lakini sio kubaki Camp Nou bila kusaini mkataba mpya aliopewa.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe