Rangnick Kupewa Timu Moja Kwa Moja?

Baada ya kuiongoza Man United kwenye michezo 10, inasemekana, uongozi wa United unamfikiria Ralf Rangnick kama kocha wa muda mrefu.

Rangnick alipewa kazi ya kuiongoza Manchester United kwa miezi 6 kama kocha wa mpito wakati huu ambao viongozi wanaendelea na mchakato wa kumtafuta kocha wa kudumu.

Matokeo uwanjani yameimarika kwa kiasi chake. Kwenye EPL, United wameshinda michezo 5, sare 2 na kupoteza mchezo 1. Wametoka na clean sheet kwenye michezo 4. Pamoja na hilo, Ralf ameifikisha United kwenye mzunguko wa 4 wa Kombe la FA na pia, Man United ipo kwenye nafasi ya 4 kwenye msimamo wa EPL kwa sasa.

Rangnick

Kunafununu kuwa, bodi ya wakurugenzi wa United imesimamisha mchakato wa kumtafuta kocha wa kudumu na sasa, wanamuangalia Ralf kwa ukaribu zaidi kuona timu hiyo itakua na matokeo gani kuelekea mwishoni mwa msimu.

Inadhaniwa kuwa, endapo United watafanya vizuri ndani ya miezi kadhaa iliyobaki kabla ya msimu kuisha (wakimaliza kwenye top 4 na kutwaa taji lolote msimu huu), kuna uwezekano kilichotokea kwa Solskjaer kikajirudia kwa Rangnick.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe