Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 42, Ashleigh Barty anakua raia wa kwanza wa Australia kufika hatua ya fainali ya mashindano ya Australian Open.
Barty ambaye ni bingwa wa Wimbledon, anatinga hatua ya fainali baada ya kumburuza Madison Keys kwenye mchezo wa nusu fainali kwa matokeo ya seti 6-1 6-3.
Christine O’Neil ndio mwanamke wa kwanza (raia wa Australia) kutwaa taji la Australian Open, ilikuwa mwaka 1980.
Kwa matokeo haya, Ashleigh Barty atachuana na Danielle Collins kwenye fainali ya Australian Open jumamosi hii.
Collins anatinga fainali baada ya kumzidi uwezo Bingwa wa French Open (2020), Iga Swiatek kwa matokeo ya seti 6-4 6-1. Hii ni mara ya kwanza kwa Collins kucheza fainali ya Grand Slam kwenye maisha yake ya kucheza tenesi.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.