Klabu ya Barcelona wana mda hadi Mei 31 kufanya maamuzi juu ya hatma ya Oscar Mingueza klabuni hapo.
Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa klabu imeamua kutumia kipengele cha kuongeza mkataba wa staa huyo moja kwa moja kilichokuwepo kwenye mkataba wake.
kwa mujibu wa Diario Sport, Barcelona wameamua kuongeza mkataba hadi Juni 2023, huku mazungumzo na wakala wa mlinzi huyu mwenye miaka 21 yakitarajiwa kuendelea siku chache zijazo.

Wakala Josep Maria Orobitg anatarajiwa kufanya mazungumzo juu ya hatma ya mteja wake kwa mda mrefu zaidi.
Mingueza ameweza kupenya kwenye kikosi cha kwanza cha Barcelona kwenye mechi ya Ligi ya Mabinwa dhidi ya Dynamo Kyiv, na ameweza kujijengea uaminifu kwa Ronald Koeman, huku akiwa kwenye nafasi nzuri ya kushiriki michuano ya Olympic na timu ya taifa ya Hispania.
Mingueza anaweza kucheza kama beki wa kati au kama beki wa kulia, anatarajiwa kuendelea kuwa sehemu muhimu ya Barcelona ikiwa watakamilisha mpango huo.
Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.



Venerose
Mmmh
Sarah
Duuh
Adelta
Wako sahii
warda
Mingueza anajua sana