Klabu ya Barcelona Inaripotiwa kuwa kwa sasa haijajiandaa kuyafikia mahitaji ya kimkataba ya Chelsea kwa mlinzi wake Antonio Rudiger.
Wiki iliyopita, ilidaiwa kuwa wawakilishi wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani walikutana na maofisa wa Barcelona kujadili uwezekano wa uhamisho wa majira ya joto.
Huku Rudiger akiwa amebakiza chini ya miezi mitatu kwenye mkataba wake Stamford Bridge, anatarajiwa kuwa mchezaji huru na anaweza kufanya majadiliano na vilabu vya kigeni.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Sport, Barcelona hawana nia ya kumlipa Rudiger kiasi cha jumla cha €7m (£5.88m) kwa msimu, pamoja na ada ya kusajili.
Ingawa Barcelona wanajulikana kuwa katika soko la kutafuta angalau beki mmoja mpya wa kati, inapendekezwa kwamba wataendelea tu na dili la mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ikiwa yuko tayari kukubali ofa ya cha chini zaidi.
Kocha mkuu wa Chelsea Thomas Tuchel alisisitiza Ijumaa kwamba bado ana uhakika wa kusalia na huduma ya Rudiger kwa muda mrefu.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.