Haaland Kufanya Maamuzi Mwisho wa Mwezi

Mshambulizi wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland anaripotiwa kuwa atafanya uamuzi kuhusu mustakabali wake mwishoni mwa mwezi huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akihusishwa kwa sehemu kubwa na kuhamia Real Madrid, ambayo itakabiliwa na ushindani kutoka Manchester City na mahasimu wao wa La Liga Barcelona kuwania saini ya chipukizi huyo.

Vilabu vyote vitatu vinasemekana kuwa vilifanya mazungumzo na wakala Mino Raiola na babake Haaland, na kandarasi zote zinaeleza wazi suala la michezo na kiuchumi ambayo Haaland atanufaika nayo.

Kwa mujibu wa Sport, Haaland anataka kuondoka Dortmund kwa heshima kwani ana uhusiano mzuri na klabu na mashabiki, hivyo atawasiliana na timu hiyo ya Ujerumani kwanza kuhusu uamuzi wake.

Kifungu cha kuondoka cha pauni milioni 63 kwenye kandarasi ya sasa ya Mnorwei huyo pale Signal Iduna Park lazima kianzishwe kabla ya Aprili 30, ndiyo maana Haaland ataamua kati ya Los Blancos, Barca au Man City ifikapo mwisho wa mwezi huu.

Katika misimu yake miwili na nusu akiwa Dortmund hadi sasa, Haaland amefunga mabao 80 katika mechi 83 alizoichezea klabu hiyo, na kuvunja rekodi ya magoli kwa Ligi ya Mabingwa.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.