Mshambuliaji wa Paris Saint- German Kylian Mbappe amesisitiza kwamba bado ahajafanya maamuzi ya kama ataendelea kuichezea PSG au ataondoka kwenda Real Madrid mwisho wa msimu huu.
Mbappe aliongea na waandishi baada ya ushindi wa 5-1 dhidi ya Lorient siku ya Jumapili ambapo mchezaji huyo machachari wa Ufaransa alihusika katika mabao yote matano akifunga mara mbili na kusaidia mengine matatu ambayo yalifunga na Neymar (2) na Lionel Messi (1).
Mbappe aliripotiwa kuzipiga chini ofa za PSG mara mbili na ilisemekana atajiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa bure lakini PSG wanataka kumbakisha winga huyo wa miaka 23 sasa ni jinsi gani atasalia na muda wake umeisha huko Paris ni watampa mkataba wa muda mfupi ili kuilinda thamani yake.
“Sijafanya maamuzi lakini kuna vitu vipya kwa sasa. alisema Kylian Mbappe
“Kama ningefanya uamuzi ningesema, mara nyingi nipo mbele. Sina haja ya kuficha. Ninataka kufanya uamuzi bora iwezekanavyo. Lakini si uamuzi rahisi.”
Kisha akaulizwa: “Je, inawezekana kubaki PSG? akajibu Ndiyo, bila shaka.”
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.