Kocha wa zamani Manchester United na Barcelona Louis van Gaal amebainisha kwamba anapambana na saratani ya tezi dume, sasa vilabu hivyo vikubwa barani Ulaya vilimtumia ujumbe wa faraja na kumuunga mkono katika jitihada za kupambana na ugonjwa huo.
Van Gaal aliwahi kuifundisha Barcelona kutoka mwaka 1998 -1999 na kufanikiwa kutwaa taji la LaLiga wakati pia alikuwa meneja wa United mwaka 2016 na kufanikiwa kushinda FA Cup.
Barcelona walisema: “Mawazo na maombi yetu yanaenda kwa meneja wa zamani wa Barca, Louis van Gaal, ambaye amegundulika kuwa na saratani ya tezi dume. Kuwa imara, Louis, na upone haraka.”
United walituma salamu zao za heri, wakisema: “Kila mtu katika Manchester United yuko nyuma kabisa ya meneja wetu wa zamani, Louis van Gaal, katika vita vyake dhidi ya saratani. Tunakutumia nguvu na ujasiri, Louis “
Van Gaal kwa sasa anaifundisha timu ya taifa ya uholanzi ambao wamepangwa kundi moja na Qatar, Senegal na Ecuador katika michuano ya kombe la Dunia 2022.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.