Barcelona Yavizia Watatu Ligi kuu ya Uingereza.

Klabu ya Barcelona inaelezwa wanavizia saini za wachezaji watatu katika ligi kuu ya Uingereza katika dirisha dogo la mwezi Januari mapema baada ya kupita michuano ya kombe la dunia.barcelonaMiamba hiyo ya soka nchini Hispania imepanga kuboresha eneo la kiungo la klabu hiyo ndo maana anatafuta saini za viungo watatu kutoka ligi kuu ya Uingereza wakiongozwa na kiungo wa klabu ya Chelsea Jorginho raia wa Italia.

Klabu ya Barcelona ambao wanashika nafasi ya pili kunako ligi kuu ya Hispania huku wakiwa kwenye hatihati ya kutofuzu hatua ya 16 bora kwenye ligi ya mabingwa ulaya huku timu hiyo ikonekana bado haijakaa sawa chini ya kocha Xavi.barcelonaViungo wengine ambao Barcelona inawatolea macho ni Youri Tielemans kutoka Leicester na Ruben Neves kutoka Wolverhampton Barca wanahitaji wachezaji hawa ili kuimarisha timu hiyo na kuirudisha kwenye ubora wake.

Miamba hiyo ya Catalans kupitia rais wake Laporta ambae alisema wataingia sokoni Januari kuboresha kikosi chao hivo tutarajie lolote kutoka kwenye klabu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.