Mchezaji wa klabu ya Manchester City Benjamin Mendy amechiwa huru kurudi uraiani kutoka mahabusu kwa dhamana alipowekwa baada ya kushitakiwa kwa kesi za ubakaji na unyanyasi wa kingono
Benjamin Mendy amekuwa akishutumiwa na kesi zinazofwatana ambazo zinahusu ubakaji na unyanyasi wa kingono kwa mabiti wadogo, ameachiwa huru leo kwa dhamana baada kusikilizwa kwa shauri lake kwenye mahakama ya Chester Crown Court leo Ijumaa.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa timu ya Ufaransa aliwekwa kizuizini kwa siku 134 tangu akamatwe kwa mara ya kwanza na kushitakiwa mwezi august mwaka uliyopita, awali alikuwa anashikiliwa kwenye gereza la Liverpool kabla ya kuhamishiwa kwenye gereza la jijini Manchester na kupatiwa dhamana na jaji Patrick Thompson kwenye shauri binafsi.
Benjamin Mendy alijiunga na klabu ya Manchester City mwaka 2017 akitokea klabu ya nchini Ufaransa AS Monaco kwa ada ya £52 million lakini alisimamishwa na klabu hiyo baada ya kushitakiwa ili kupisha uchunguzi.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.


