Benzema Afikia Rekodi ya Ronaldo.

 

Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema ameendeleza ubabe wake hapo jana na kufikia rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo Cristiano Ronaldo baada ya kufunga magoli 3 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Chelsea.

 

Karim Benzema

Benzema alifunga magoli 3 “hat-trick” yake ya pili mfululizo katika michezo ya Ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya PSG na Chelsea na kufikia rekodi iliyokuwa akishikiliwa na Ronaldo alipofanya hivyo dhidi ya Bayern na Atletico mwaka 2017 alipokuwa akiitumikia Blancos.

Benzema alifunga magoli yake katika dakika ya 21′, 24′ na 46′ katika dimba la Stamford Bridge hapo jana baada ya kufanya hivyo dhidi ya PSG katika mchezo wa 16 bora wiki kadhaa zilizopita.

Mchezo wa marejeano baina ya timu hizo utachezwa Jumanne ijayo katika dimba la Santiago Bernabeu ambapo vijana wa Tuchel wana kibarua cha kupindua meza ilikuweza kufuzu katika hatua ya nusu fainali.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe