Brazil Bado Wanamuhitaji Ancelotti

Timu ya taifa ya Brazil imeonesha bado haijakata tamaa kwa kocha wa Real madrid Carlo Ancelotti ambae wanataka aifundishe timu ya taifa ya nchi hiyo akirithi mikoba ya kocha aliyepita Tite.

Shrikisho la soka nchini Brazil CBF limeripotiwa kufanya mazungumzo na Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez wakihitaji kocha Ancelotti achukue mikoba ya kocha Tite, Shrikisho hilo limeeleza kua lipo tayari kusubiri mpaka msimu umalizike ili waweze kumuajiri kocha huyo.BrazilTaarifa kutoka nchini humo zinaeleza kua kocha Ramon Menezes ambaye ni kocha wa nchi hiyo chini ya miaka 20 ataisimamia timu hiyo kwa kipindi cha muda mfupi, Huku wakiwa tayari kumsubiri kocha huyo mpaka mwisho wa msimu huu.

Shrikisho la soka nchini Brazil limekua ikimfatilia kocha Ancelotti kwa kipindi cha miezi miezi miwili sasa tangu kumalizika kwa michuano ya fainali za kombe la dunia, Huku aliyekua kocha wa timu hiyo Tite kuondoka kwenye timu hiyo mapema baada ya fainali hizo kumalizika.BrazilShirikisho la soka nchini Brazil inaelezwa kwasasa linataka kumuajiri kocha wa viwango vya dunia ambaye atakua mzawa kwakua nchi hiyo imeshindwa kuzalisha makocha wenye viwango vya dunia, Lakini vilevile makocha wazawa wameonekana kutokufanya vizuri kwa miaka ya karibuni.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.