Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Anchelotti ameeleza kua golikipa wake namba moja wa klabu Thibaut Courtois atakosekana katika pambano la El Clasico litakalopigwa jumapili katika dimba la Santiago Bernabeu.
Siku kadhaa nyuma kocha huyo alifunguka na kusema anamtarajia golikipa huyo kurejea katika mchezo wa El Clasico baada ya kukosa michezo kadhaa nyuma kutokana na majeraha lakini bahati mbaya hatakuepo pia kwenye mchezo huo.
Kocha huyo amefunguka kipa wake huyo anaendelea vizuri kwasasa lakini hatakua tayari kwenye mchezo huo wa jumapili labda siku kadhaa mbele anaweza kua sawa zaidi.
Wakati huo Mukraine Andriy Lunin golikipa namba mbili wa klabu hiyo anatarajiwa kusimamia milingoti ya Real Madrid katika mchezo huo kuendelea kukaimu nafasi ya Courtois ambaye ataendelea kuugulia majeraha katika mchezo huo.
Carlo Anchelotti kikosi chake kinaadamwa na majeruhi baada ya beki wake Antonio Rudiger kupata majeraha katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya katikati ya wiki na haijafahamika bado kama ataweza kuwepo kwenye mchez huo wa jumapili.
“Ni mchezo muhimu,Lakini sio maisha au kifo. Msimu ni mrefu sana. Ingawa ni Wazi tungependa kushinda mchezo huo” Carlo Anchelotti akiongelea mchezo huo utakaopigwa siku ya jumapili

