Soka ni mchezo wa wazi ambao linalofanyika mara nyingi huonekana wazi kabisa bila kificho. Hilo linadhihirika wazi kabisa ndani ya klabu ya Liverpool ambao wanafanya vyema sana ndani ya ligi kuu ya Uingereza. Uimara wa kikosi chao ni chachu kubwa sana ya ubingwa kwao kwa msimu huu na hapo mbeleni.

Katika siku za nyuma Liverpool hawakuwa klabu inayotazamwa sana kiushindani lakini baada ya kuwasili kwa Klopp mambo yalianza kubadikika ghafla sana kikosini hapo na kuona kabisa mambo yaliyokuwepo hapo awali yanaanza kubadilika na kuwa kama yake yaliyokuwepo miaka ya nyuma sana ndani ya kikosi hicho.

Mabadiliko makubwa sana yamefanyika ndani ya kikosi hicho hakika jambo ambalo mara nyingi lilikuwa linaonekana kama ndoto kuja kutokea ndani ya kikosi hicho. Lakini kwa sasa mtu anapotaja Liverpool anamaanisha mabingwa wa klabu bingwa barani Ulaya ambayo ni mafanikio makubwa kwa Klopp.

Kiwango cha Liverpool kwa wakati uliopo sio moto unaoweza kuzimwa kizembe bali ni nguvu ya muda meefu inaweza kuondoa mfumo imara uliopo ndani ya kikosi hicho. Hiyo inatokana muda mrefu ambao wameweza kutumia katika kukijenga kikosi hicho ambacho kina manufaa ya kiushindanj kwa baadae.

Nyota anayekipiga na klabu ya Arsenal, Ceballos ambaye ana msimu mmoja pekee ndani ya ligi hiyo ya Uingereza anaonesha kuweza kuwakubali Liverpool kwa aina ya soka wanalolicheza katika mechi zao. Liverpool wanacheza mchezo wa kasi sana ambao unawapa shida sana wapinzani kujipa nafasi ya kujiachia hata kidogo.

Anasema unapocheza nao unahitaji utimamu wa aina yake kutokana na kukulazimisha mara kadhaa kuwa langoni kwako jambo ambalo kama umakini wako upo chini lazima utawaruhusu waweze kukushambulia kwa kasi ya ajabu na kukuacha ukiwaruhusu waweze kukufunga vile watakavyo wao.

Ni timu yenye muunganiko mkubwa ambao unaonekana kusumbua hata kwa zaidi ya misimu mitatu mbeleni kwa sababu aina ya wachezaji ambao Klopp yupo nao umri wao unawaruhusu kufanya makubwa zaidi kwa mbeleni.

Akiwa kama mchezaji anasema hajatokea kuona klabu inagusa sana mpira wa kasi kama Liverpool na hilo analitamani sana. Kiuhalisia Liverpool ndio washindani wakubwa msimu huu na watawasumbua sana hata Manchester City ambao wanapewa nafasi zaidi ya kunyanyua vikombe.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa