Nyota wa klabu ya Barcelona walionesha upendo wao wa pekee mbele ya nyota mwenzao Neymar katika kipindi cha usajili ili kuweza kumsaidia kurejea upya kujiunga nao baada ya maisha yake ya Ufaransa kuonekana hayaendi vile ambavyo yeye alitazamia yangeweza kwenda kwa kipindi ambacho alikuwa hajajiunga na klabu hiyo.
Jitihada hizo zote ilikuwa ni kutoa sehemu ya malipo ya mshahara wao ili kuweza kumsaidia na kuisaidia klabu kuweza kuweka vitabu vyao sawa na kukusanya pesa ya kutosha ambayo klabu ya PSG walikuwa wanaihitaji ili kumwachia nyota huyo kurejea ndani ya kikosi chake hicho cha zamani.
Japo pia iliweza kufahamika kwamba kuna baadhi ya watu kikosini hapo hawakutaka kabisa kurejea kwa nyota huyo raia wa Brazil kwa namna mambo yake yalivyokuwa yanaratibiwa kwa yeye kuweza kurejea klabuni hapo. Hiyo inasemekana ni kutokana na sababu za nyota huyo kuondoka katika mazingira ambayo wao hawakupendezwa nayo.
Pique na Messi ni miongoni mwa watu wa karibu sana wa mchezaji huyo na walitamani sana kurudi kwa nyota huyo ndani ya jiji hilo. Pique ndiye aliyeweka mambo wazi kwamba walipambana kwa namna fulani; yeye na nyota wenzake kuweza kuomba kupunguziwa mishahara yao ili kuchangia uhamisho wa Neymar aweze kurudi.
Neymar alijaribu kutaka kujitahidi kurejesha mikoba yake Hispania mara baada ya miaka miwili pekee ya kuwatumikia PSG katika uhamisho ambao ulivunja rekodi ya dunia na uliweza kugharimu kiasi kikubwa sana cha pesa ambacho ni £222m. Pesa ambayo Barcelona waliipokea kutoka kwa mauzo hayo.
Anasema yeye na baadhi ya wachezaji wenzake waliweza kumweleza wazo lao Raisi wa klabu hiyo kwa kuona kwamba hata vitabu vyao vya klabu visingekaa vema wakafikia hatua ya kutoa sehemu ya malipo yao kwa kusema waliamini kiasi hicho kingerudi kwa miaka miwili au zaidi na kuomba kubadilishiwa mikataba ili kuchangia uhamisho huo japo halikufanikiwa.
Lakini nyota hao walipojojiwa hivi karibuni juu ya endapo nyota huyo kama ataweza kurejea kikosini hapo, aliweza kusema kwenye soka kila jambo linaweza kutokea lakini akaongeza kwamba kabla ya Neymar kuondoka waliweza kumshauri kwa kumwambia anakwenja katika gereza la dhahabu bila kujua: lakini ushauri wao haukuweza kuchukuliwa.
Furahav
Noma sana.