Ronaldinho: Picha Halisi ya Maisha ya Kiamerika Kusini!

“Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni!” hii ni methali ya Kiswahili yenye maana tamu na nzuri ya kutuaminisha kuwa maajabu hayaishi abadani, kila uchwao kuna vituko vipya vinatokea ambavyo kwa vyovyote vile utabaki kinywa wazi. Ila hili la Ronaldinho Gaucho wengi limetuacha kinywa wazi. Nguli huyo wa soka amekamatwa katika nchi ya Paraguay akiwa na kitambulisho na vyeti vya kughushi ili kuingia katika nchi ya Paraguay, ajabu amesema alikuwa hajui kuwa ni vya kughushi, haahaahaa, huu si utani huu!

Ila dunia hii, hivi unapata wapi ujasiri wa kumfanyia hivi Gaucho. Kwani nani asiyemjua Ronaldinho katika dunia hii, huyu mwenye tuzo za Ballon d’Or, huyu anayepiga chenga za utashi wa hali ya juu, huyu huyu ambaye mabeki akiwa na mpira wanaogopa kumfuata, yaani huyu huyu ambaye picha zake hadi kwenye makaratasi ya pipi na gum yupo daaaah, halafu kuna mtu anakuja kumuingiza kingi kizembe (anamtapeli), ama kweli kila mbabe ana mbabe wake.

Kiujumla Ronaldinho anatuonesha tu kuwa nyani ni nyani tu ata umvalishe suti, tai, viatu na miwani, pengine hili suala ni kweli au sivyo ila mhhh. Waamerika Kusini wana maisha ya ajabu kidogo bila kupepesa macho ni wapenda starehe. Kule kuna wauzaji na watengenezaji wa madawa ya kulevya, heroine na cocaine, ule usela wa kuchomana visu, ukahaba, maisha ya kulipiana visasi, ujuaji mwingi, utapeli, kamari, kumbi na fukwe za starehe. Ajabu ni kuwa wananchi wengi ni masikini hivyo njia za panya ni nyingi katika upatikanaji wa kipato. Wengi waliobahatika ni wachezaji wa soka na waliofanikiwa zaidi wanatoka Amerika wanaenda mabara mengine kutafuta pesa na kweli wanazipata.

Ubaya unakuja pale ambapo wanapokuja kuzitumbua fedha hizo na marafiki zao wa zamani ambao wengi ni wahuni na wameshazoea maisha hayo, Luis Suarez ni muathirika mkuu wa kuwa na marafiki wahuni huko Uruguay. Luis Adriano naye alikuwa hivi hivi huko kwao yeye na pombe klabu na yeye Ronaldo de Lima hadi huyu Ronaldinho hivi hivi tu huko Brazil.

Kuna mahali natetea ukamatwaji wa Ronaldinho na kaka yake aitwaye Roberto. Kwani wao walipewa mualiko kwa ajili ya kuangalia watoto wasiojiweza na kwenda kuwaonesha kitabu chake huko nchini Paraguay, hati na kadi za kusafiria zote walipewa na Dalia Lopez. Wao kazi yao ilikuwa ni kusafiri tu, na cha pili ni kuwa walipita uwanja wa ndege salama pasi na kugundulika na kuingia katika jiji la Asuncion. Baadaye wakaja kukamatwa wakiwa kwenye vyumba vyao vya mapumziko, hapo ndiyo ninapoamini kuwa mtengenezaji wa hati na kadi hizo alikuwa mtaalamu kweli kweli yaani mapolisi wa uhamiaji hawakuzijua kwa urahisi.

Ipo haja ya Ronaldinho na kaka yake kujitetea. Ronaldinho alishikwa mapema mwanzoni mwa mwezi huu wa tatu na dhamana yake imekataliwa. Mwanasheria wake bwana Queroiz amesema kuwa Ronaldinho atakoka kwa sababu yeye hakujua kuwa hati hizo za kusafiria ni za kughushi.

Japokuwa amekamatwa ugenini lakini bado Ronaldinho amepewa heshima zote, anaishi katika jela nzuri yenye viwango vyote, jela ambayo hufungwa wale wafungwa maarufu wenye heshima zao.Waziri wa mambo ya ndani wa Paraguay amesema chumba anachokaa Ronaldinho gerezani ni kama hoteli, pia, anapewa uhuru wa kucheza mpira na kama kawaida yake unajua nini anafanya. Katika mechi iliyochezwa siku tatu zilizopita Ronaldinho amecheza mechi akiwa gerezani na kushinda mabao matano na kupika mengine sita hivyo kukamilisha ushindi wa 11-2 katika kiwanja kidogo cha gerezani.

Ukaguzi uliofanyika mnamo Machi 13 nyumbani kwa Daila Lopez umebaini kuwepo kwa mipira mingi yenye picha za Ronaldinho, picha hizo zinafanana kabisa na ile picha iliyopo kwenye kitambulisho cha bandia. Hivyo inawapa walakini askari wa Paraguay kuhisi kuwa mpango mzima wa kutumia vitambulisho feki Ronaldinho na kaka yake wanaufahamu. Ikiwa Ronaldinho atakutwa na hatia basi itamlazimu akae jela kwa muda usiopungua miezi sita. Ronaldinho akiwa selo amesikika akimuuliza mwandishi kuwa ni muda gani atakaa humo na akaapa hatokuja kukanyaga tena nchi hiyo.

Uzuri ni kuwa hata akiwa huko selo bado Ronaldinho wetu anatabasamu muda wote. Wafungwa wanafurahi kuwa naye, mapolisi ndiyo usiseme. Naamini kuna watu dua zao zimekubaliwa hapa, Haaahaah! Aaaa, amini usiamini hivi nani hatamani kukutana na Ronaldinho? Nani hatamani kucheza naye timu moja? Au nani hatamani kupiga stori mbili tatu na Ronaldinho? Japokuwa tunaombea Corona ipite ila Ronaldinho tumkumbuke walau kidogo tu.

Ubaya ni kuwa wafungwa wanaomba afungwe ili wabaki naye tegerezani na siye tunaomba tuonane uraiani. Basi shaghalabaghala, patamu hapo!

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.