Hii ni Changamoto kwa LeBron

Wahenga husema ‘Kizuri siku zote hurushiwa kila aina ya uchafu’. Kauli hii inakuja kutokana na kile kinachodaiwa kwamba kwa asilimia kubwa wakongwe wengi wa mpira wa kikapu hawapendezwi na kitendo cha LeBron kujiita mchezaji mkubwa wa muda wote kama anavyoitwa na wengi [G.O.A.T- Greatest player Of All Time], na yeye mwenyewe kujibatiza hivyo.

James akiwa anaendeleza ile kaulimbiu yake aliyoipa jina la ‘Zaidi ya mwanamichezo’ [More than an Athlete]; inaonekana kuwakera sana wakongwe wengi waliowahi kucheza na kuhisika kwa namna moja au nyingine kwenye mchezo huo wenye historia kubwa sana duniani.

James alichangia kwa kiasi kikubwa pale alipowapa kikombe na kuzima kiu ya miaka 52 kwa timu hiyo kukosa ubingwa kwenye ligi hiyo ya NBA. Anasema “kuna wakati niliwahi kuonesha hisia zangu za ndani kabisa ndani ya mchezo huu, niliweza kutoa machozi kwa kile kilichotokea baada ya kuzima kiu ya Cavaliers ya miaka 52; hii inanifanya niupende sana mchezo huu na kujiona bora”

Baadhi ya wakongwe kama  Kevin McHale na Isiah Thomas wao wanabeza kile anachokiita James kuwa ni mafanikio ambayo yamechagizwa kwa kiwango kikubwa na weledi wake na kujituma katika mchezo huo awapo uwanjani. Wao wanaona hakuna kipya kwake na kwamba mafanikio yakipangwa kutokea yanatokea haijalishi nani anakuwepo kwa wakati huo; hivyo kwao hakuna kubwa ambalo wanaona mchezaji huyu amelichangia hadi kujiita mchezaji bora wa muda wote.

Thomas anaendelea kusema “huku ni kukoseana heshima kabisa kuna wachezaji wengine walifanya zaidi ya makubwa kipindi chao, na wewe unaanza kujifananisha nao: huwezi kufananisha nyakati zile na hizi kwa sababu ni vitu viwili ambavyo haviendani. Kuna kitu kinachomfanya mtu bora sio kwa namna hii anayoisemea James. Sijawai kumuona Michael Jordan akijisema yeye ni bora au ni mchezaji bora wa muda wote, japo anaweza kujisemesha mwenyewe ila sio kujitangaza”.

Kitu hicho kimeendelea kuwatoa jasho baadhi ya wakongwe wa mchezo huo kwa kujiona kama nafasi zao zinakosewa, na wao wanapoteza ile hadhi yao waliyokuwa nayo na mchango wao katika timu kionekana kama haukuwa na kitu baada ya jina LeBron kukua kwa kiwango kikubwa katika vyombo vingi vya habari.

Tukirudi katika uhalisia LeBron ni mchezaji mkubwa ambaye amefanya kila linalofanywa na yeyote anayestahili kuitwa mkongwe kwenye tasnia hii. Mafanikio yake ni makubwa na sio ya kubezwa; kwa umri wake wa miaka 34 bado anaonekana ana kitu kikubwa cha kufanya mbeleni hata kwa miaka minne zaidi kwa kasi hiyo hiyo. Hivyo, kumfananisha na watu kama  Bill Russell, Kareem Abdul-Jabbar, Michael (Jordan), Larry (Bird) na Magic (Johnson) ni kitu ambacho ni cha kawaida sana.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.