Mashetani Watatu wa Mashetani Wekundu

Ole Gunnar Solskjær amekuwa kipenzi cha mashabiki wengi wa klabu hiyo na anasifiwa kwa mapinduzi makubwa ya kisoka aliyoyaleta ndani ya klabu hiyo. Kitu ambacho kinapendwa zaidi na mashabiki wa klabu hiyo ni nafasi aliyoichukua timu hiyo na kuifanyia mabadiliko makubwa sana ambayo siyo rahisi kwa mwalimu mwingine kuweza kubadili mapokeo ya wachezaji haraka vile na kuanza kunusa mafanikio ndani ya muda huo.

Pamoja na kuwasili kwa kishindo lakini, bado kuna wachezaji ambao wanapata shida sana kuendana na mfumo wake kitu ambacho kinaweka hatiani maisha yao ya kisoka ndani ya klabu hiyo. Fellaini amekuwa akipata shida sana kuendana na mambo ambayo mwalimu huyo amekuwa akiyataka kuyaona kwenye kikosi chake hivyo amekuwa na mazingira magumu sana kuenenda na mifumo hiyo. Ila, wapo wachezaji ambao kiuhalisia wamebadilishwa kabisa na mwalimu huyo:

Paul Pogba

Kwa sasa amekuwa sio yule aliyekuwa akionekana kama alipotea kutua katika kikosi hicho, amekuwa aina ya wachezaji ambao wamebadili mfumo mzima wa timu na wao wenyewe kubadilika. Amepata nafasi ambayo kwa hali ya kawaida anajiona mwenye furaha siku zote ndani ya kikosi hicho na kupitia kitu hicho ndipo anaonekana kukua zaidi kisoka. Kwa sasa maisha yake ndani ya klabu hiyo ni ya kicheko tu hana wasiwasi juu ya nafasi yake. Kwa 55% amehusika na magolo 20 yaliyofungwa na klabu hiyo akiwa na magoli sita na pasi za magoli 5 chini ya kocha huyo. Ole amempa imani ya kufanya vizuri ndio maana anaona matunda hayo.

Marcus Rashford

Hadi sasa ana magoli nane katika mechi 13 za hivi karibuni alizocheza. Ameshika nafadi ya ushambuliaji vilivyo na kumfanya mtangulizi wake aliyeaminiwa sana na Mourinho, Lukaku kusugua benchi kutokana na makubwa anayoyafanya uwanjani. Kwa sasa ni mchezaji anayetumainiwa ndani ya kikosi hicho na kuona ni kizazi cha baadae ambacho kitakuwa na nafasi ya kufanya vizuri zaidi ya ilivyo sasa. Wengi wanamwona mchezaji huyo kama amevaa tayari viatu vya Ronaldo ndani ya kikosi hicho japo bado ni mapema mno kumpa heshima ya namna hiyo. Kwa umri wake na anachokifanya ana nafasi ya kufanya makubwa zaidi ya hayo.

Anthony Martial

Maisha ya klabuni hapo kwa sasa yamemshawishi hadi kusaini kandarasi mpya ambayo inampa nafasi ya kendelea kusalia kikosini hapo. Anerejea kwenye nafasi yake ya awali na uwezo wake umekuwa ukibadilika kadri siku zinavyokuwa zinasonga mbele. Wakongwe wa klabu hiyo wamemtabiria makubwa zaidi mchezaji huyo na kuona kwamba ana nafasi ya kufanya zaidi ya ilivyo sasa na wanaonekana kurejesha kizazi cha Manchester ile ya Ferguson ambayo ilikuwa haishikiki kabisa.

3 Komentara

    Kocha bora.

    Jibu

    Kocha Hana huwez wachezaj wanajitoleah tu

    Jibu

    Man United ni klabu kubwa sna na ilikuwa ipo vzr Sana kipindi cha Ferguson hivyo hinatakiwa kocha ole Gunnar inabidi wakaze buti yy na wachezaji wake wairudishe timu ya mashetani wekundu km ilivyokuwa awali

    Jibu

Acha ujumbe