Kapteni wa klabu ya Chelsea ameripotiwa kukubaliana na klabu ya Barcelona kujiunga nayo ambapo mkataba wake utakapo malizika na timu yake ya sasa mwisho wa msimu.
Cesar Azpilicueta alijiunga na Chelsea akitokea klabu ya Marseille inayoshiliki ligi kuu ya Ufaransa miaka kumi iliyopita, pia amefanikiwa kushinda mataji nane likiwemo taji la ligi ya mabingwa Ulaya, katika kipindi chote alichokuwepo kwenye viunga vya Stamford Bridge.

Thomas Tuchel na klabu ya Chelsea hawana wasiswasi kuhusu swala la mkataba, wanatarajia Cesar ataamua hatma yake mwenyewe baada ya klabu kumpa mkataba wa muda mfupi, lakini Azpilicueta amefanya mazungumzo na klabu ya barcelona na wamekubalina lakini hajasaini mkataba wowote mpaka sasa.
Chelsea inaweza kuwapoteza Antonio Rudiger, Andreas Christensen na Cesar Azpilicueta kutokana wachezaji wote watakuwa huru kusaini mikataba ya awali na klabu yeyote.
Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

CHEZA HAPA

