Mchakato wa kuiweka klabu ya Chelsea sokoni, huenda ukaingiwa na kirusi ambacho pengine kitatoa taswira tofauti na inayotarajiwa.

Chelsea iliwekwa sokoni mwishoni mwa mwezi Machi na aliyekua mmiliki wa klabu hiyo – Roman Abramovic ambaye alitaka dau la £2.5B ili kuiachia timu hiyo. Pamoja na dau hilo, Abramovic aliripotiwa kutoidai timu hiyo kiasi cha £1.5B ambayo aliikopesha. Hata hivyo, pesa ya mauzo ya klabu hiyo awali alipanga ipelekwe moja kwa moja kwa waathirika wa vita ya Ukraine kupitia kitengo cha misaada cha klabu hiyo.

Muda mfupi baadae, serikali ya Uingereza ilitangaza kuzifungia mali zote za bilionea huyo zilizopo nchini Uingereza ikiwa ni pamoja na mchakato wa kuiuza klabu hiyo. Vikwazo kadhaa vimewekwa kwa klabu hiyo ikiwa ni pamoja na kupewa leseni maalumu ya kuendesha timu hiyo mpaka Mei 30,2022.

Chelsea, Chelsea: Kirusi Kuharibu Mpango., Meridianbet

Wakati utaratibu wa kuinunua klabu hiyo ukiendelea, kumeibuka hali ya sintofahamu. Inaripotiwa kuwa Abramovic sasa anataka kulipwa deni aliloikopesha timu hiyo (£1.5B). Awali alijitolea kuliacha deni hilo lakini, baada ya vikwazo anavyoendelea kuwekewa na serikali ya Uingereza, bilionea huyo amebadilisha mawazo na anataka kulipwa kilicho chake.

Pamoja na deni la Abramovic, kumezuka maswali mapya kuhusu pesa itakayolipwa na mnunuzi mpya wa Chelsea itatumika katika misingi ipi? Nani atahusika na kupokea na kutumia pesa hiyo wakati huu ambao serikali imeingilia kati ikiwa na matakwa binafsi dhidi ya Abramovic.

Chelsea, Chelsea: Kirusi Kuharibu Mpango., Meridianbet

Mchongo unaweza kuungua zaidi endapo leseni ya Chelsea itakwisha muda wake angali suluhu haijapatikana katika mchakato huu. Baraza la EPL litakaa Juni 8, 2022 kuanza mipango ya msimu ujao. Kama the Blues watakua bado wapo kwenye mfumo huu wa kiundeshaji, kuna kila dalili hawatohusika kwenye mipango ya EPL kwa msimu ujao kwani hawatambuliki nje ya leseni waliyonayo.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa