Niwaambieni kitu kuhusu kisa cha Daudi na Goliath, najua mnajua maana mmesoma sana vitabu, Ila Daudi hakutaka kutumia nguvu zaidi ya akili najua mnajua nani alishinda kwenye vita ile.
Niwaambieni nini kuhusu somo la historia, madaftari nimetupa ila topic ya Crisis in the Capitalist world sijaisahau kabisa, vita ya kwanza ya dunia Wajerumani walipigwa vibaya sana.
Mkataba wa Versailles Peace treaty pale Ufaransa, wajumbe wote walimkandamiza sana Ujerumani Ila alitakiwa mtu mwenye akili tu kurejesha tumaini la Ujerumani, nani mwingine kama sio Poster Boy Adolph Hitler.
Dunia imeshahama kwenye matumizi ya mabavu tangu zamani kwenye umri wa mabadiliko (reinnasence age) waliwapenda wakina Albert Einstein, Isaac Newton na wakina Galillei Galilleo, na sio mabavu na nguvu kwenye Kila kitu, niamini Mimi.
Clatous Chama, amesafiri mbele ya muda, najua unajua nazungumzia Time Travelling ni elimu kubwa sana, Chama alishaishi Zama za nyuma Sana, zama ambazo soka lilikuwa linatoka kwenye matumizi ya nguvu na kuja kwenye akili.

Chama bila shaka haishi kwenye dunia ya sasa, Ila amesafiri kuja kutukumbusha namna Zvonmir Boban alikuwa anakitakatisha kiungo, ametuletea kitabu cha Diego Maradona cha dimba la Aztecta pale Mexico.
Wakati anaondoka kwenye dunia yake, kwenye begi lake Mama yake hakumfungia maandazi Bali kitabu cha Agustin Azuka Okocha ‘Anko Jay Jay’ alivyokuwa anawasambaratisha Wajerumani na kuondoka na mabeki kumi na mbili kisha chuma matata mbele ya Oliver Kahn, mpaka leo ndio bao bora Bundesliga.
Pass yake ya jana haikuwa maelezo mengi inaitwa backheel assist au No Look Assist, iliwahi kupigwa na Fundi Ferensc Puskas kwenye usiku wa baridi kali pale Austria wakati Real Madrid anakiwasha kwenye UEFA, vitu vile viliwahi kufanywa nyuma, nawe umevileta tena.

ASANTE, Clatous Chama asante kwa kuja, laiti kama ningejua ujio wako usiku wa jana kabla ya kesho basi ningemwambia Babu yangu akusubiri, akupigie ngoma za kwetu Wangindo Liwale Lindi.
FURAHIA KASINO YA MTANDAONI
Tembelea ardhi ya maajabu ushangazwe na mengi ikiwa ni pamoja na urahisi wa kujipatia utajiri kupitia Kasino ya Meridianbet.


lombo
asante meridianbet kwa habar moto moto
aisha
Simba mko vizuri sana pia sisi mashabiki tunatambua uwepo wenu
Amiri Kayera
Ni mchezaj anaefany mpila uonekan lahisi
Sadick
Ni moja ya usajiri bora kabisa kutoka nje ya nchi. Hivyo ndivyo wachezaji wanaotoka nje waonyeshe uwezo kama Chama ili wenyeji wajifunze#meridianbettz
Rehema
Good news 👍
Saupha mohamed
Usajili mzuri ..simba itazidi kuaimara
Janeflora malisa
Nice
Hopemwaikuka
Chama ni balaaa lingne
Neema
Habari yakuvutiaa
Issa
Ni safi ila wamepata wanyonge
Sabrina
Chama yuko vizuri
felister
ni moja ya usajili bora
Dorophina
Chama anaisaidia sana simba kufika mbali
Mwanahamisi
Chama Yuko vizuri
Sauda
Wachezaji wanatakiwa kujifunza kupitia kwa Chama
Frank P
Huyu chama ni fundi aisee
Nasra
Gud news
Mwajumah
Chama ni balaa lingine
Caroline
Chama Kama chamaa
Fatina mfigi
Cham na mkubali sana
Tahiya
Wachezaji wa nyumbani jifunzeni kupitia chama mwamba wa lusaka
Salma ngende
Habari nzuri
Angelina
Yuko vizuri
magdalena
chama sijaona kama ana mpinzani wa kumzidi kimpira apa tanzania kijana anajua na yupo makini sana
Gabriel
Kwaida sana
Zeiyana
Chama hana kipaji kikubwa sana katika Mpira ila ndio ivyo tena hana nyota
Khadija
Kawaida sana
Rose kapinga
Chama kaja kazini kwel,mfano wa kuigwa!!
Ernest
Mwandishi inaonekana unajuwa kuwakera sana watu
Tatu
Chama mtu hatari
JULIANA WILBARD ALEX
Chama kijana machachali,anajua
David Pere
Ni moja ya usajiri bora kabisa kutoka nje ya nchi. Hivyo ndivyo wachezaji wanaotoka nje waonyeshe uwezo kama Chama ili wenyeji wajifunze