Pambano la UFC 249 lililopangwa kufanyika mwezi wa nne mwaka huu na kutangazwa na Raisi wa UFC Dana White lingefanyika, limeahirishwa baada ya kampuni ya kurusha matangazo ya (ESPN) na (Parent Company Disney) kumzuia Raisi wa UFC Dana White kuendelea na mpango wake wa kuendeleza mapambano hayo licha ya janga la Korona (Covid19)
Mara baada ya pendekezo la kuendelea na pambano kutoka, White alitangaza maamuzi ya kufunga makubaliano yake na ESPN ambao ni chombo cha Habari washirika wa UFC wenye mkataba wa zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni moja na nusu.
Pambano la UFC 249 lilipangwa kufanyika mwezi wa nne tarehe 18 na lingefanyika katika Kisiwa lakini White hakutaja kingekua ni kisiwa gani.
Kwenye mahojiano na vyombo vya habari White amesema “nilipigiwa simu na Viongozi wa juu wa Disney na wakaniambia niahirishe mipango yangu ya kuendelea na kuliandaa pambano la tarehe 18”
Mshindi wa UFC uzito wa kati kwa wanawake Rose Namajunas aliomba kuahirishwa kwa pambano lake dhidi ya Jessica Andrade kutokana na vifo vya ndugu zake wawili kufariki kutokana na maambukizi wa virusi vya Korona (covid19).


Mariam mtandama
Corona inatisha jamani