Messi Amewatema Inter, Ni Barca tu!

Nyota Lionel Messi amekataa taarifa zinazomuhusisha na klabu ya Inter Milan, na kudai kuwa hana mpango huo.

Nyota huyu alianza kuhusishwa na klabu hiyo ya Inter baada ya raisi wa zamani wa klabu hiyo kusema kuwa ndoto ya Inter kumpata Messi inawezekana. Messi pia alikuwa anahusishwa na klabu yake ya zamani ya Old Boys ya Argentina.

Messi amezungumzia taarifa zote mbili ya kuhusishwa na klabu ya Inter Milan na Old Boys. Amesema taarifa hizo zote ni za uwongo, na anashukuru mashabiki wake wake hawaamini taarifa hizo.

Messi alibainisha kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la kuongezeka kwa taarifa za uongo kuhusu hatma yake klabuni Barcelona. Licha ya taarifa kuwa alikuwa na mvutano na viongozi wa Barca lakini Sky Sport waliripoti kuwa ana mpango wa klabuni hapo.

Taarifa zinataja kuwa klabu ya Barcelona inatarajia kukaa mezani na staa huyu ili kufikia maridhiano ya kuongeza mkataba wa Lionel Messi kwa miezi ijayo, lakini hali ya sasa ya uchumi inatia wasi wasi kulingana na Janga la virusi vya corona.

3 Komentara

    Anajua atapoteza mvuto ndo maana ataki messi wa baka tu

    Jibu

    Huyu messi kanywa maji ya Barca.

    Jibu

    Lion messi anaangalia masilahi sana ameona kuwa huko hatakuwa zaidi na pia hata akibaki Barcelona bado yutabaki kuwa mashabiki wake

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.