Daniel James Kuamua Nafasi Yake United

Wakati mashabiki wa Man United wakisubiri kuona msimu ujao unakwendaje, baadhi ya wachezaji wanamaamuzi ya kufanya, Daniel James ni mmoja wao.

James alijiunga na United mwaka 2019 akiwa miongoni mwa wachezaji watano wa kwanza kusajiliwa (akiwemo Harry Maguire, Aaron Wan-Bissaka, Bruno Fernandes na Odion Ighalo) na Ole Gunnar Solskjaer.

Maisha ndani ya United, yamekuwa ni safari ya kupanda na kushuka kwa Daniel James, hii imemfanya winga huyu kukosa namba ya kudumu kwenye kikosi cha timu hiyo.

Man United imekamilisha usajili wa Jadon Sancho, kuongezeka kwa winga huyu, kunaongeza ushindani wa nafasi kwenye kikosi hicho na huenda James akaathirika zaidi kwa kukosa namba kwa muda mrefu.

Ni dhahiri kuwa, James anahitaji kucheza mara kwa mara. Kwa sababu hiyo, dirisha hili la usajili ni fursa pekee ya James kuondoka United. Leicester City na Leeds United zinahusishwa na usajili wa winga huyu raia wa Wales.

Leeds United sio wageni katika mbio za kuiwania sahihi ya James, walifanya hivyo msimu uliopita bila ya mafanikio. Manchester United wameweka thamani ya £15M kwa timu yeyote inayomtaka winga huyo.


VUNA MKWANJA NA KASINO ZA MERIDIANBET!

Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe