Golikipa wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Hispania David De Gea amefunguka kua yupo kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Klabu ya Manchester ipo kwenye mazungumzo ya kumuongezea mkataba golikipa huyo alieitumikia klabu hiyo kwa mafanikio klabu hiyo. De Gea mkataba wake unakaribia kumalizika ndani ya timu hiyo na mashetani wekundu wanataka kumbakiza golikipa huyo.
Klabu ya Manchester United kwa siku za karibuni wamekua wakifanya mazungumzo na wachezaji wao muhimu klabuni ili kuwaongezea mikataba waendelee kusalia klabuni hapo, Ukiachana na golikipa huyo Man United ipo kwenye mazungumzo na mshambuliaji wake Marcus Rashford, Diogo Dalot, pamoja na kiungo Fred.
Golikipa David De Gea anasema anaamini mazungumzo yake na klabu hiyo yataisha kwenye uelekea mzuri, Huku akisema ana matumaini ya kumaliza maisha yake ya soka ndani ya klabu ya Manchester United kwani hiyo ni klabu yake na anafurahia kuwepo hapo.
David De Gea ni mchezaji pekee ndani ya kikosi cha manchester United anayepata nafasi ambaye alikua kwenye timu ya kocha mwenye mafanikio klabuni hapo Sir Alex Ferguson. Na hiyo ni kutokana na uwezo ambao amekua akionesha msimu hadi msimu.

