Kiungo wa FC Barcelona Frank De Jong amedai kuwa “siku zote alitaka kusalia Barcelona” licha ya kutakiwa na Manchester United wakati wa dirisha la usajili la msimu huu wa 2022/2023.

 

De Jong: Daima Nilitaka Kubaki Barcelona

Mchezaji huyo ambaye ni raia wa Uholanzi alikumbwa na sakata la muda mrefu, huku kocha wa zamani wa kiungo huyo wa Ajax Eric Ten Hag akiripotiwa kuwa na hamu ya kujenga kikosi chake kipya cha United akiwa na mchezaji huyo karibu.

Ilionekana uwezekano wa kuhama baada ya kudaiwa kuwa De Jong alikuwa anadaiwa Euro milioni 17 katika mishahara iliyoahirishwa na kutakiwa kusaini mkataba mpya na kupunguzwa kwa mishahara ya karibu asilimia 40.

Badiliko hilo halikufanyika ingawa, United badala yake walimsajili Casemiro kutoka Real Madrid kwania ya kuimarisha safu yao ya kiungo. Akizungumza kwenye majukumu ya Kimataifa wiki hii, De Jong alikiri si kila kitu kilikwenda sawa kati yake na Barca, Lakini hakuwahi kufikiria kuondoka Camp Nou.

 

De Jong: Daima Nilitaka Kubaki Barcelona

“Siku zote nilitaka kusalia Barcelona, na hii ndiyo sababu nilibaki mtulivu wakati mtulivu wakati wa kiangazi;. Mchezaji huyo wa miaka 25 alisema. Siwezi kutoa mengi, lakini angalia klabu ina mawazo yake na nina mawazo yangu pia, na wakati mwingine hii inagongan. Lakini mwisho wa siku, mambo yalikwenda sawa.

De Jong ni sehemu ya kikosi cha Uholanzi kwaajili ya mechi zijazo za Ligi ya Mataifa dhidi ya Poland na Ubelgiji.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa