Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ufaransa Didier Deschamps amesema kuwa kumchukua Paul Pogba ambaye yupo nusu fiti ni jambo lisilowezekana kuelekea michuano ya kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika Qatar November mwaka huu.

 

Deschamps Kuhusu Majeraha ya Pogba

Deschamps na Ufaransa ambao ni watetezi wa kombe hilo amesisitiza kuwa hatamchukua nyota huyo wa Ufaransa baada ya majeraha aliyoyapata na kuondolewa kwenye mechi kadhaa za Mataifa. Pogba bado hajaonyesha ushindani mpaka sasa  tangu arejee Juventus kwa uhamisho wa bure mwezi Julai.

Mchezaji huyo ambaye ni mshindi wa kombe la Dunia 2018  ana shaka kushikiriki michuano hiyo nchini Qatar  baada ya kuamua kufanyiwa upasuaji ili kutatua jeraha la meniscus kwenye goti lake la kulia. Mchezaji huyo si tuu peke yake anayeleta wasiwasi kwa kocha huyo kabla ya Mashindano ya ligi ya Mataifa ya Austria na Denmark mwezi huu.

 

Deschamps Kuhusu Majeraha ya Pogba

Pia nyota wa Real Madrid Kareem Benzema nae ameachwa nje ya kikosi baada ya kupata jeraha la goti, ingawa Carlo Ancelloti anasema kuwa mchezaji huyo “anaendelea vyema” wiki hii, wakati huo huo N’golo Kante, Presnel Kimpembe, Lucas Hernandez, na Kingsley Coman pia wako nje.

Lakini jeraha la Pogba ndilo linalotia wasiwasi zaidi kwa Deschamps, ambaye hakuweza kutoa taarifa zozote kuhusu hali yake siku ya Alhamis. Alisema,

 

Deschamps Kuhusu Majeraha ya Pogba

“Haiwezekani leo kuthibitisha chochote isipokuwa kupitia kuingilia itifaki ya matibabu aliyonayo”  Ninamfahamu vyema Paul, ambaye nazungumza nae mara kwa mara. Leo hii, hakuna mtu hata yeye amaeweza kusema kuwa atakuwepo kwenye Kombe la Dunia. Sijui kama anaweza kuponywa.

Deschamps aliendelea kusema kuwa kama atapona itakuwa ni jambo zuri hata hivyo hawezi kuja akiwa hajapona kwani kuna wachezaji ambao watakuwa tayari kucheza. Kukosekana kwa Benzema kunamaanisha kuwa Griezmann anaweza kupewa nafasi ya kuanza kwenye michezo ijayo ya Les Bleus licha ya kuona muda wake wa kucheza kwenye klabu ni mdogo, ambapo watacheza Septemba 22 na Austria na baadae watacheza na Denmark siku tatu baadae.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa