Earling Haaland ni Kama Mwenge Tu.

Earling Haaland mshambuliaji wa klabu ya Manchester City raia wa Norway ambaye kwasasa yupo kwenye kiwango bora kabisa, Jana aliendelea alipoishia mwisho juma dhidi ya mahasimu wao Manchester United.

earling haalandEarling Haaland kwasasa amekua kama mwenge tu kwasababu mwenge unapita kila kijiji na Haaland anafunga karibia kila timu anayokutana nayo,Hii ni baada ya jana kufunga mabao mawili katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Fc Copenhagen kwenye ushindi wa mabao matatu kwa bila walioupata klabu ya Manchester City.

Mshambuliaji huyo amekua na kiwango bora toka ajiunge na wananchi wa jijini Manchester majira ya joto na kua tishio zaidi kwa timu pinzani kwa namna anavyofunga mabao mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22.

Haaland amefikisha mabao 19 usiku wa jana baada ya kucheza michezo 11 ikiwa ni rekodi nzuri sana kwenye upande wake huku akiendeleza ubora wake kwenye kila mchezo anaoingia kiwanjani.

earling haalandEarling Haaland amekua akipokea maoni kutoka kwa magwiji mabalimbali wa soka duniani wakisifu ubora wake ambao anauonesha hivi sasa, Kama Gwiji wa zamani wa klabu ya Liverpool na Ajax Luis Suarez ambaye amemtaja mchezaji huyo kama namba tisa bora kwasasa duniani.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.