Emery: Chelsea Inaendelea Vizuri Chini ya Potter

Kocha mkuu wa Aston Villa Unai Emery amemuunga mkono Graham Potter kwa mafanikio ya muda mrefu akiwa Chelsea na anasema tayari kuna dalili za maendeleo Stamford Bridge.

 

Emery: Chelsea Inaendelea Vizuri Chini ya Potter

Potter alimrithi Tuchel kwenye dimba la Chelsea mapema Septemba, lakini mustakabali wake ulitiliwa shaka kufuatia ushindi mmoja katika mechi 11 zilizoanza mwaka huu.

Hata hivyo, kocha huyo wa zamani wa Brighton and Hove Albion amebadilisha mambo taratibu, huku Chelsea ikiingia kwenye mapumziko ya kimataifa kwa kushinda mara tatu na kutoka sare moja.

Mkufunzi wa Villa Emery, ambaye alidumu kwa miezi 18 Arsenal kabla ya kutimuliwa Novemba 2019, anaamini Potter anastahili kabisa nafasi yake ya kung’ara katika klabu kubwa.

Emery: Chelsea Inaendelea Vizuri Chini ya Potter

Emery amesema kuwa; “Alifanya vizuri sana akiwa na Brighton na anahitaji muda kurekebisha mawazo yake akiwa Chelsea. Taratibu, wanafanya vizuri zaidi na bora zaidi, kazi ya Tuchel pia ilikuwa ya kushangaza, lakini kile Potter alifanya na Brighton kilikuwa cha kushangaza sana na alistahili kuchukua hatua na timu kama Chelsea.”

Sasa wanaendelea. Kila kitu alichofanya awali akiwa na Brighton anaweza kufanya vilevile akiwa na Chelsea. Anahitaji muda tu wamecheza vyema kwenye Ligi ya Mabingwa lakini hawajakuwa na msimamo katika Ligi Kuu. Lakini tunajua kesho tunacheza na moja ya timu bora kwenye Ligi Kuu. Ni changamoto nzuri kwetu na hii ndiyo sababu niko kwenye Ligi Kuu. Aliongeza Emery.

Villa wamefikisha pointi 10 kutoka kwa pointi 12 walizocheza, na kuwaacha sawa kwa pointi na wapinzani wao Chelsea walio katika nafasi ya 10, na Emery sasa analenga kumaliza kipindi cha kwanza.

Emery: Chelsea Inaendelea Vizuri Chini ya Potter

Kocha huyo amesema kuwa sasa wanaweza kufikiria changamoto yao mpya ambayo ni kuwa katika 10 bora na hii itaanza kesho na wanafikiria kuwa wana uwezekano mzuri kuwa huko.

“Mechi nne zilizopita tulizocheza, tukifunga mabao saba na kufungwa moja pekee, kushinda mechi tatu na kutoka sare moja, ulikuwa wakati mzuri sana kwetu.”

Acha ujumbe