Epl Yatoa Orodha ya Wanaowania Tuzo za Kocha Bora wa Mwezi.

Epl ligi kuu ya Uingereza imtoa orodha rasmi ya makocha watakaowania tuzo ya kocha bora wa mwezi wa nane ikiwa imejumuisha makocha watano.

Ligi kuu ya Uingereza wana utaratibu wa kutoa tuzo kwa kocha bora kila mwezi ambae hua anapata tuzo hiyo kutokana na mafanikio ya timu yake ndani ya mwezi huo na makocha hao ni Pep guardiola wa Man city,Mikel arteta wa Arsenal,Graham potter wa Brighton, Marco silva wa Fulham, pamoja na Antonio conte wa klabu ya Tottenham.

Hawa makocha wote wameziwezesha timu zao kupata matokeo mazuri ndani ya mwezi wa nane tukianza na Arteta ambae yeye alivuna alama 15 ndani ya mwezi wa nane na kufanikiwa kushinda michezo yote mitani ya mwezi huo huku Pep yeye kwenye michezo mitano ya awali alishinda michezo minne na kusuluhu mmoja huku akiwa sawa na Antonio Conte wa Spurs huku Graham potter kwenye michezo mitano ya awali ndani ya mwezi agosti alishinda mitatu,kufungwa mmoja na kusuluhu mmoja huku mwalimu wa Fulham United iliopanda daraja yeye kwenye michezo mitano ya awali akiwa ameshinda michezo miwili,kusuluhu miwili na kufungwa mchezo mmoja hivo kufanya timu yake kukusanyan alama 8.

Kwa utaratibu uliopo kura zitapigwa kupitia tovuti za ligi hiyo kuchagua kocha bora wa mwezi ndani ya ligi hiyo kuzingatia vigezo ambavyo huwekwa.

Acha ujumbe