Eriksen Achukizwa Kukaa Benchi

Kiungo wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Denmark Christian Eriksen amefunguka kua anachukizwa na yeye kutokupata muda wa kucheza ndani ya klabu hiyo kwasasa.

Kiungo Eriksen amesema ameongea na kocha Erik Ten Hag juu ya yeye kutofurahishwa kusugua benchi na kumuambia anahitaji muda wa kucheza mara kwa mara.eriksenKocha Erik Ten Hag amemueleza kiungo huyo kua kwasasa Mainoo anafanya vizuri, lakini pia viungo wengine klabuni hapo wanafanya vizuri hivo kuna ushindani wa nafasi kwenye eneo la katikati.

Msimu uliomalizika kiungo huyo alikua akipata nafasi mara kwa mara ndani ya kikosi cha kwanza cha Man United. Lakini mambo yameonekana kua tofauti msimu huu kwani amekua akitumia muda mwingi benchi kuliko uwanjani.eriksenKiungo Eriksen kwasasa amekua chaguo la tatu ndani ya kikosi cha Man United jambo ambalo haonekani kufurahishwa nalo, Huku akisisitiza yeye anahitaji zaidi muda wa kucheza ndani ya kikosi hicho.

Acha ujumbe