Eriksen Amerejea Rasmi

Kiungo wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Denmark Christian Eriksen amerejea rasmi ndani ya klabu hiyo baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Eriksen amekaa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitatu kwani kiungo huyo ameumia tangu mwezi wa kwanza katika mchezo wa kombe la Fa dhidi ya Reading, Kitu kilichomfanya mchezaji huyo kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu lakini hatimae mchezaji huyo amerejea rasmi kwenye mazoezi ya timu hiyo na timu ya kwanza.EriksenKiungo huyo aliripotiwa kurudi kwenye timu hiyo wiki moja nyuma lakini hakua ameweza kufanya mazoezi na wenzake, Siku ya jana mchezaji huyo ameonekana akifanya mazoezi na wachezaji wa klabu hiyo hivo kuonesha ni rasmi sasa amerejea ndani ya klabu hiyo.

Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari kuhusu mchezo wa kesho dhidi ya Everton na kusema habari nzuri ni kua kiungo Eriksen amerejea kwenye kikosi na atakuwepo kwenye sehemu ya kikosi kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Everton.EriksenChristian Eriksen amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya Manchester United na kua msaada mkubwa sana ndani ya timu hiyo kabla ya kupata majeraha, Hivo kurejea tena kwa kiungo huyo inakua ni habari njema kwa mashabiki wa klabu hiyo kutokana na kiwango ambacho alikua anakionesha kiungo huyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.