Christian Eriksen amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa tisa ndani ya klabu ya Manchester United na kuwashinda wachezaji wenzake kama Raphael Varane pamoja na Jadon Sancho.

Nyota huyo raia wa Denmark amefanikiwa kunyakua tuzo hiyo baada ya kucheza kwa kiwango cha hali ya juu katika michezo ya mwezi wa tisa ndani ya klabu hiyo na kupigiwa kura na mashabiki wa klabu hiyo kua bora zaidi baada ya klabu hiyo kutangaza mapema mchana wa leo.

eriksenHii imekuja siku moja baada ya Christian kufunga bao zuri akiwa katika majukumu ya timu yake ya taifa kwenye michuano ya Uefa Nations League dhidi ya timu ya taifa ya Croatia.

Kiungo huyo ambaye amekua na kiwango bora tangu ajiunge na timu hiyo kwa uhanisho huru akitokea klabu ya Brentford amekua miongoni mwa wachezaji muhimu zaidi katika kikosi hicho cha mashetani wekundu chini ya mwalimu Eric Ten Hag.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa