United Wamewasiliana na Ernesto Valverde?

Manchester United wanaripotiwa kuwa wanafikiria kumchukua aliyekuwa kocha mkuu wa zamani wa Barcelona Ernesto Valverde.

United wanatafuta meneja mpya baada ya kumtimua alyekuwa meneja wao Ole Gunnar Solskjaer wikiendi iliyopita.

The Reds wameanza vyema msimu huu baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu msimu uliopita na kutumia pesa nyingi msimu wa joto, lakini hali imekuwa tofauti wiki chache zilizopita wakirekodi matokeo mabaya kwa gemu kadhaa.

Safari ya kumsaka bosi mwingine imehusisha malegendari kama Zinedine Zidane na Mauricio Pochettino.

United Wamewasiliana na Ernesto Valverde?

Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, United imefanya ‘mawasiliano ya moja kwa moja’ na kocha wa zamani wa Barcelona, ​​Valverde.

Valverde amekuwa nje ya kibarua tangu alipoondoka Barcelona mwaka 2020, ingawa kwa makusudi, bosi huyo wa zamani wa Barcelona aliamua kupumzika.

United inaweza kuwa changamoto kwake, lakini kwa mujibu wa ripoti, atachukuliwa tu kama chaguo la muda.

The Reds wanasemekana kuwa tayari kuajiri bosi wa muda hadi mwisho wa msimu, ingawa haijulikani ikiwa Valverde angefikiria kuchukua jukumu kama hilo kwa muda.


PANDISHA THAMANI YA DAU LAKO NA FAI CAI SHEN

Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.