LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga leo ametua nchini Tanzania akitokea nchini Ubelgiji alikokuwa kwa ajili ya mapumziko ya lazima yaliyotokana na Virusi vya Corona.
Eymael ametua Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na baadhi ya Waandishi wa Habari ambao walikuwepo hapo.
Licha ya taarifa zake za kurejea leo kuwa wazi hakukuwa na mwakilishi yoyote wa Yanga ambaye alikuwa alikuwepo uwanjani hapo.
Kocha huyo anatarajiwa kuungana na wachezaji wake kesho, Shinyanga ambao wamekwenda huko kujiandaa na mchezo dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa Juni 13.
Habari zinaeleza kuwa majukumu yalikuwa mengi kwa viongozi wa Yanga siku ya leo.
“Kuna mmoja amepewa likizo na wengine wapo na timu kwenye msafara hivyo kesho mambo yatakuwa sawa,” ilieleza taarifa hiyo.
Magdalena
Karudi awafundishe vyema wachezaji wake ili timu ifanye vizuri ipande viwango
warda
Yaani vyura fc bwana kocha ndo kaingia leo ha haaaaaa#meridianbettz
Elika
Yanga kwa sasa hawana jipya..nawashauri wajipange upya
Ernest
Hii inamaana gani, kocha anarudi bila ata mapokezi??!! Mambo ya Bongo haya
isha
Duuh bongo noma sana
Ester jackson
Bora amerudi mana vijana walijiachia sana mpaka uzitu umeongezeka
Aziza mushi
Duh hii Nina Sana jmn anarudi ata mapokezi hakunaaπ€
Aziza mushi
Duh hii noma Sana jamani anarudi bila ya mapokeziπ€
Neema juma
Afadhalii karudii ili wachezajii waongeze bidii zaidi
Asia Abdy
Duh kazi ipo
Neema hassan
Kocha mahiri sana
Zeiyana
Sio kuwafundisha tu kuchukua ubingwa kabic yanga ya wanachi
mwakalosi
utopolo janja janja nyingi si hivyo katumiwa tickets katua nnchini
Emmy cleopa
Ahsante kwa taarifa
Sylvester
Karibu kwenye timu yako mbovu mjiandae vipigo tu mwanzo mwisho
Tahiya
Karibu tena bongo naona umekuwa mwenyeji ndio mana ukupokelewa
Povel
Ni habar njema kwa wapenzi wa jangwan na wapenda soka thnks meridian bet kwa update za michezo
Rehema Dickson
Karibu tuanze mapinduzi yetu tupondue meza kombe lije nyumbani jangwan
Gabriel
Habar njema kwetu wanayanga
Theonestina
Habari njema kwa wenye chama lao
Frank Patrick
Araf akapanda daladala airport pale kuelekea kkoo jangwani
Ester mmakasa
Karibu bongo eymael jangwani ndo kwako sasa .
Lydia Emmanuel Magoti
Duu noma Sana kocha katua ata mapokez mazuri hamna haya karibu kwenye timu yako mbovu upambane nayo
Caroline
Karibu sana
David Pere
Karudi kuendeleza ushindi au kufungwa
Furahav
Kalibu kumalizia ligi.