Adres Iniesta - Mgeni Aliyevikwa Ufalme wa Katalunya

Historia yake ilianzia kijiji kimoja La Fuentealbilla kwenye jimbo la Albacete, Castille Le Mancha huku wengi tukipenda kumuita Mkimbizi wa La Masia kwakua alikua miongoni mwa watoto wachache kutokea nje ya Jimbo la Catalunya.

Andres Iniesta akishangili kwa kuvua jezi ili kuonesha Heshima kwa rafiki yake

Iniesta kwenye umri wa miaka 12 wakati anapelekwa Chuo cha soka La Masia, hakuwa na furaha alilia sana kuachana na rafiki zake kijijini, kuachana na wazazi wake kisha kuanza maisha mapya Catalunya, muda mwingi alikua mkimya na mtu mwenye aibu sana.

Lakini Kocha wa timu ya vijana enzi hizo Enrique Orizola aliona kipaji kikubwa kwenye miguu yake, alianza kama Kiungo wa Ulinzi, kabla ya kusogea kiungo Mshambuliaji, winga na kiungo wa kati, kote Iniesta pale Chuoni alikuwa balaa tupu

Iniesta akiwa mazoezini ili mlazimu Pep Guardiola amwambie Xavi kuwa, “Najua utanistaafisha hapa, ila yule mtoto Mkimbizi atatustaafisha wote, wewe na mimi” balaa tu mazoezini

Ule msimu wa 2004-05, Iniesta alipata namba kikosi cha wakubwa, alikuja kuwa muhimili wa Barca, Frank Rjkaard alimtumia kama straika wa pili, akamshusha kama Kiungo wa kati na bado kama winga ila Iniesta alikua anatembea kama hana akili nzuri.

Iniesta na Dani Jarques

Ndani ya Iniesta kulikua na Michael Laudrap, huyu Babu alikua fundi wa style ya La Croqueta, hii ni aina ya kukokota mpira kwa kuchezesha miguu, mpira unatoka kulia kwenda kushoto, sasa Iniesta aliifanya ila kwa speed mara mia zaidi ya Laudrup

Iniesta akiutambuka msitu wa mabeki ilikua zaidi ya burudani, Wahispania wakampachika jina El Caballero Palid yaani kisu kikali kinacho kata na kufukua misitu ya mabeki wa timu anazokutana nazo.

Iniesta alipitia wakati mgumu sana msimu wa 2009/10 msimu huu alimpoteza rafiki yake Dani Jarques, walicheza wote timu za vijana za Spain, licha ya Dani kuwa Espanyol walikua marafiki sana, kifo chake kilimfanya aharibikiwe kisaikolojia na kupoteza hamu ya soka
.
Ililazimika Watalaam waajiriwe kumuweka sawa, ndio maana alivopiga kamba dhidi ya Uholanzi pale Sauzi alivua shati na kumpa ujumbe rafiki yake “Always with us Dani Jarque”, aliamini rafiki yake alipo anatazama kazi zake.

3 Komentara

    Anajua sanaaa

    Jibu

    Yuko vozuri

    Jibu

    Iko vizuri

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.