Pape Diouf ndie alikua Raisi wa kwanza Mweusi wa klabu zinazo shiriki ligi kuu nchini Ufaransa. Raisi huyo raia wa taifa la Senegali aliongoza Marseille kati ya mwaka 2005 hadi 2009 kipindi ambacho timu hiyo ilichukua nafasi ya pili ya ligi kuu na kushiriki fainali za kombe la Ufaransa mara mbili. Na ulipofika mwaka 2010 walichukua ubingwa wa ligi baada ya miaka 18.

Pape Diouf amefaliki akiwa na umri wa miaka 68 baada ya kukutwa na maambukizi ya Virusi Korona (COVID19). Timu hiyo imeripoti “Pape atabaki mioyoni mwa wana Marceille milele, kama moja ya watu walio itengeneza historia ya timu yetu” Marseille walipost ujumbe huo kwenye kurasa zao za mitandao ya jamii.
Bodi ya mchezo wa mpira wa miguu wa kimataifa ya nchini Ufaransa (L.F.P) imesema “ Tumepoteza Muandishi, Wakala, Na Raisi wa Olympique Marseille, Pape amehudumu maisha yake yote kwenye mpira wa miguu, kwetu alikua ni mwanachama wa LFP tangu Septemba 2007 mpaka juni 2009 Tutamkumbuka Pape kama muhisani na kiongozi mwenye Tija ”

Mchezaji wa zamani wa Liverpool Djibril Cisse aliwahi kuitumikia Marseille kipipindi ambacho Pape anaiongoza timu hiyo amesema. “Leo mota wa Ufaransa umepoteza mtu muhimu, Maumivu yangu ni makubwa mno pumzika kwa amani”


Furahav
Hongera sana.
aisha
R.I.p
Sabrina
R.I.P