"Hatukupendi" -Dyabala kwa Ronaldo

Paulo Dyabala anasema kuwa aliwahi kumwambia mwanatimu mwenzake wa sasa, Christiano Ronaldo kuwa watu Argentina hawana mapenzi na yeye, yaani hawampendi na hakuwa maarufu kwao.

Dyabala anabainisha kuwa alimwambia hivyo Cristiano Ronaldo ba kumlinganisha na Lionel Messi. Kwa mujibu wa Dybala watu wa Argentina walimpenda nyota mzawa Lionel Messi na walikuwa wakimchukia Ronaldo.

Ikumbukwe kuwa upinzani kati ya Ronaldo na Messi kwenye soka umekuwa ukigonga vichwa vya habari karibu kila siku kwa kuwa wamekuwa mfano na kivutio kwa wadau wengi wa soka. Wote kwa pamoja wamekuwa ni wachezaji wenye mashabiki wengi sana ulimwenguni. Ushindani wao haswa ulikuwa kipindi Ronaldo alipokuwa akichezea Real Madrid.

Ushindani wa dimbani kati ya Ronaldo na Messi ulifika tamati baada ya Roldao kutua Juventus mwaka 2018, lakini mijadala ya nani bora na takwimu zikiendelea kuchukua nafasi kwa wingi.

Maneno ya Dyabala

“Nilimwambia [Ronaldo] tunakuchukia kidogo kule Argentina, Tunakuchukia kwa sababu ya maumbile yako, namna ulivyo, unavyotembea. Lakini ukweli ni kuwa umenishangaza kwa kuwa nimegundua upo tofauti”

Dyabala ni mmoja kati ya wachezaji wachache waliopata bahati ya kucheza na mastaa hawa wote wawili, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Hivyo kwa nafasi yake ameweza kuwajua wachezaji wote na kuweza kuwatofautisha katika vipengele kadhaa.

Acha ujumbe