HAWA NDIO  WACHAMBUZI WA MICHEZO YA  FIFA

Kwa wafuariliaji wa soka la Uingeleza na la Ulaya kiujumla majina ya Martin Tailor na Alan Smith yanaweza yakawa sio mageni kwao, Lakini pia yawezekana ukawa mfuatiliaji na usijue watu hawa wananogesha vipi utamu wa soka kwa mbwembwe na ueledi wa aina yake katika kutangaza na kuchambua soka. Urafiki wa watu hawa ni wa zaidi ya miaka 9, ambapo tarehe 30 mwezi juni Alan Smith alitangazwa na Easport kua mrithi wa Andy Gray na yeye kua mwenza wa Martine Tailor katika kuingiza Sauti kwenye michezo inayotengenezwa na Easport maarufu kama (Fifa playstation games)

Martin Tailor kushoto akiwa na Alan Smith

Martine Tailor ni mtangazaji wa mpira wa miguu wa nchini uingeleza na Mkurugenzi msaidizi wa timu ya mpira wa miguu ya Woking na alizaliwa tarehe 14  septemba mwaka 1945 mjini Chester nchini Uingereza. Na amefanya kazi kama mtangazaji na mchambuzi wa mpira katika kituo cha habari cha Sky Sport tangu mwaka 1990, akitangaza mashindano mbali mbali ikiwemo Ligi Kuu nchini Uingeleza , Ligi ya mabingwa Ulaya pamoja na michezo ya kimataifa.

Alan Smith aliezaliwa tarehe 21 Novemba mwaka 1962 na kutumikia vilabu kadhaa vya nchini Uingeleza ikiwemo Leicester City mnamo mwaka 1982 na kufunga magoli 13 kwa msimu wake wa kwanza kabla ya kukimbilia Arsenal mwishoni mwa mwaka 1987 ambako alijipatia umaharufu mkubwa baada ya kufunga goli tatu peke yake katika mchezo wa Arsenal Dhidi ya Portsmouth. Alan Smith  kwa sasa ni mchambuzi msaidizi pia kwenye kituo cha televisheni cha Sky Sport na amefanya kazi na Martin Tailor katika kuchambua fainali za mapingwa ulaya.

Kuungana kwa wataalamu hawa ambao kila utakapo Anza kucheza MIchezo ya Fifa ni lazima utasikia sauti zao wakijitambulisha kumekua na mvuto mkubwa kiniashara kiasi cha wawili hao kuendelea  kutumika na EAsport mpaka ilipotoka toleo jipya la mwaka 2020.

3 Komentara

    Asante meridian sikuyajua hayooo

    Jibu

    Nawakubali sana hawa.

    Jibu

    Wako vizuri

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.