Michuano ya Ligi Kuu ya Uingereza inatarajiwa kupigwa kalenda zaidi kutokana na sintofahamu ya uwezekano wa kuendelea baaya ya April 30. Kama ligi nyingine nyingi za Ulaya, Premier League imesimama katika kukabiliana na Janga la Corona.
Klabu zote 20 za Premier League zinatarajiwa kufanya mkutano kwa njia ya video kujadili hatma ya ligi. Hakuna matumaini kabisa ya kumalizika kwa mechi hadi tarehe 30 April.
Kwa mujibu wa taarifa, Vilabu vinatarajia kukubaliana kubadili tarehe hadi mwezi Mei. Lakini pia vilabu vinaweza kubakia na uamuzi wa kufunga ligi mpaka pale hali takakapokaa sawa kama vile ligi za Hispania na Serie A zilivyoamua kufanya.
Pia katika mabo wanayohitaji kuzungumzia ni uwezekanoi wa kucheza mechi hizi katika viwanja visivyo na mashabiki.
Pia vilabu vimeshauriwa kuwa visusie Ligi, kwa kuwa kumaliza ligi mapema kunaweza ku athiri nafasi zao katika ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Adelta
Hii sio poa