Klabu ya Real Madrid inamtaka nyota anayefukuziwa na Liverpool Fabian Ruiz.
Ripoti zimetaja kuwa Real Madrid ni moja ya klabu ambazo zipo tayari kuingia kwenye mbio za kumfukuzia nyota wa Napoli Fabian Ruiz ambaye pia anatajwa kutupiwa kijicho na Liverpool.
Nyota huyu Muhispania mwenye umri wa miaka 24 ambaye aliondoka Real Betis na kutimba Italia alipoungana na Napoli, amekuwa akifanya vizuri sana na kuvutia klabu zingine.
Liverpool tayari walikuwa kwenye windo kumnasa lakini sasa wanakutana na ushindani kutoka kwa Real Madrid wakitarajia pia kumpata ili awasaidie katika safari ya matumaini kule LaLiga.
Klabu zingine zinazovutiwa na staa huyu ni pamoja na klabu ya Man United na Bayern Munich . Kwa mujibu wa wakala wa Ruiz, bwana Alvaro Torres amethibitisha kuwa ameshawasilisha kwa Napoli kuwa klabu ya Real Madrid inataka kumsajili mteja wake.


farida ahmadi
Fabian luiz hana maamuzi yake kwenda Liverpool hama Real Madrid mana zote ni klabu kubwa tyuu na nzuri pia
Povel
Gud news
Lydia Emmanuel Magoti
Itapendeza