Bruno Fernandes ni mchezaji wa soka wa Kireno ambaye anacheza kama kiungo katika klabu ya Manchester United iliyopo nchini uingereza na timu ya taifa ya Ureno. Bruno amejzolea umaarufu mkubwa nchini italiwa kwa kucheza vilabu vikubwa vya nchi hiyo vya Udinese na Sampdoria. Mshambuliaji huyo mzaliwa wa Maia nchini uleno alizaliwa tarehe 8 Septemba, na mashabiki wa Manchester tayari wameanza kumuita (the future Ronaldo) yani Ronaldo ajae. Bruno Fernandez amein’garisha Manchester United tangu alipojiunga kilabuni hapo kwa ada ya pauni milioni 68 kutoka Sporting Lispborn mwezi wa kwanza mwaka huu.

Kupoteza kwa Manchester United 2-0 dhidi ya Burnley mwezi Januari kuliumiza sana wana wa Old Trafford wakiongozwa na Ole Gunnar Solskjaer. Old Trafford ilibaki kimya kwa muda ule mpaka kipenga cha mwisho kilipo lia, lakini kukabaki mtu mmoja aliyebaki uwanjani na kusimama akionesha hisia za maumivu isiyofichika, Kocha Ole alisimama huku wachezaji wakielekea vyumba vya kubadirishia nguo.
Mashabiki walibaki na msongo, na ikawa siku isiyo na amani kwa wapenzi wa Manchester United kwa msimu wa 2019/20 na kuonekana kuautakua msimu wa maumivu na majuto kwa timu hiy, Lakini kwa sasa morali imebadirika.

Kwa wiki kadhaa tu kabla ya michezo kufungiwa kutokana na janga la Covid 19, Manchester United wameanza tena mbio za kuifukuzia nne bora ya msimamo ya ligi kuu ya Uingereza, wamefika robo fainali ya kombe la FA, na kujihaikishia hatua ya nane bora kwenye mashindani ya yuropa. Michezo yao 11 bila kufungwa ndio michezo mingi zaidi tangu kufika kwa Ole pale Old trafford.


Njiku
Bruno anaweza ila sio kumuita ronaldo wwe
Gabriel
Yuko vzur sana Bruno Fernandes
Povel
Bruno Fernandes yupo vzr chachu ya ushnd
farida ahmadi
Yuko sahihi kabisah Bruno