Ili mpira wa soka uweze kukubalika miongoni mwa wanamichezo na wapenda soka lazima kuwepo na watu wanaowashawishi kuwatazama pindi wakiwa uwanjani. Kutokana na hilo wanachangia wao kuweza kulioenda soka hilo. Pamoja na hilo kuna aina ya viungo ambao hufanya kazi ya pekee kunogesha soka hilo. Timu yenye viungo walioshibana kwa kukaa muda mrefu wana uwezo wa kufanya makubwa hata wakiwa uwanjani.
Japo wapo ambao huwa katika mfumo mmoja unaoendana hata kama hawajakaa muda mrefu kikosini hapo. Baadhi ya klabu zenye kufikia kitu hicho huweza kuwa na mlolongo mzuri sana wa matokeo wenye magoli mengi ya kufunga kuliko kufungwa.
Jorginho, Kante & Kovacic
Ingeweza kuwa Barkley ndiYo angEweza kuchukua nafasi ya Mateo lakini kutokana na kikosi kilivyo na namna ambavyo viungo hao walivyokuwa na mzunguko mzuri katika eneo la kati pindi wanapocheza; uwepo wa Jorginho ndani ya kikosi hicho unachangiza kwa kiwango kikubwa kikosi hicho kucheza mpira mwingi na wenye kuvutia.
Winks, Sissoko & Eriksen
Pochettino bila shaka alifurahia sana uwepo wa wachezaji hawa waliokuwa ndani ya kikosi cha Liverpool, walikuwa na uwezo wa kumiliki sana mpira na kutengeneza mashambulizi mengi kutokana na kasi, uimara na akili za uwanjani alizonazo Eriksen ambaye mipira yake mingi inaonekana kwa macho kwa mchezaji kuweza kufunga tu na huonekana dhahiri.
Wijnaldum, Henderson & Milner
Pamoja na uimara waliokuwanao katika safu ya ulinzi lakini eneo jingine ambalo lilikuwa tishio sana ni lile la kiungo ambacho kimekuwa muhimili mkubwa wa kukipa uhai kikosi hicho chenye nia ya kupata ushindi angalau ndani ya msimu. Uwepo wao umetia chachu na hamasa iliyokuwepo ndani ya safu mbili yaani ulinzi na ushambuliaji.
Fernandinho, Silva & De Bruyne
Kwa hakika hii ni timu ambayo ilikuwa na viungo wa kila aina yaani wale wanalipa kile kinachoonekana imani ambayo Pep aliweza kuijenga kwao. Walikuwa wakicheza aina moja ya mchezo. Ni aina ya wachezaji ambao kila kocha anawatamani.
Casemiro, Modric & Kroos
Ni nguzo pekee iliyokuwa imesalia katika kikosi hicho kwa sasa kwa wachezaji wakongwe wenye majina makubwa. Walikuwa moto wa kuotea mbali kikosini hapo kwa kufanya kikosi hicho kuonekana imara hata katika maeneo yenye mapungufu ya wazi. Kama safu ya ulinzi; uwepo wao uliweza kufuta kabisa kasoro hiyo hivi karibuni.
Issa
Mmh viungo bora