Mlinda Mlango wa Bayern Munich Manuel Neuer amemuunga mkono Yann Sommer kufanikiwa katika klabu ya Bayern Munich lakini ametilia shaka kutimuliwa kwa kocha wao wa makipa baada ya jeraha lake alilolipata baada ya kuteleza kwenye theluji.

Mkongwe huyo wa Ujerumani Neuer alipata jeraha la mwisho wa msimu kwenye mguu wake wa chini wa kulia mnamo mwezi Disemba.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 baadaye alifanyiwa upasuaji, huku tatizo hilo likija siku chache baada ya Ujerumani kutolewa katika michuano ya Kombe la Dunia katika hatua ya makundi.
Bayern walitafuta kwa kishindo kuchukua nafasi ya kipa wao nyota katika dirisha dogo la usajili la Januari, na hatimaye walifanikiwa kumleta Sommer kutoka Borussia Monchengladbach. Na Neuer “hana tatizo kabisa” nalo.

Aliliambia gazeti la The Athletic: “Niliweka picha kwenye kundi letu la WhatsApp na kuomba radhi. Mimi si mwoga ninayejificha, niliwaeleza kila kitu ikiwemo historia.”
Wakati Yann analetwa, golikipa huyo anadai kuwa aliwaambia mabosi wa klabu hiyo hana tatizo kabisa na hilo, na anafikiri ni vyema wakawa na makipa wawili wazuri. Yeye ni mchezaji wa timu na ni muhimu kwake kujua kinachotokea Bayern.
“Mimi ni sehemu muhimu ya timu na pia sehemu muhimu ya klabu na ninataka klabu na timu iwe na mafanikio iwezekanavyo. Hilo ndilo jambo muhimu zaidi kwangu. Nimemfahamu Yann kwa muda mrefu na ninajua kwamba yeye ni kijana mzuri na kipa mzuri. Klabu ilipata suluhu kubwa. Ilikuwa muhimu kwangu kwamba kuna mtu na kwamba sihitaji kuwa na wasiwasi.”

Wakati Sommer akipunguza hofu ya kipa Julian Nagelsmann, Bayern wamemfukuza kocha wa muda mrefu wa magolikipa Toni Tapalovic. Huku Neuer akisema kuwa pigo hilo limempiga sana kwani Toni alikuwa mchezaji wa timu pamoja nao na kila mtu aliona hivyo.
Na akakazia kuwa siku zote waliweza kutenganisha kazi na maisha binafsi na anaelewa kuwa inaweza kuonekana kama hana malengo au haaminiki lakini anaweza kutofuatisha. ODDS kubwa unazipata Meridianbet.

Bayern wako pointi moja mbele ya Union Berlin katika mchuano wa Bundesliga kabla ya ziara ya kesho dhidi ya Wolfsburg.

