Kocha  wa Chelsea Graham Potter anaamini kipigo cha 2-0 cha Carabao Cup hapo jana kutoka kwa Manchester City kilikuwa “hatua mbele” kwa The Blues, licha ya kushindwa kwa mara ya tatu kutoka kwa mechi nne zilizopita.

 

Potter : Kupoteza Dhidi ya City ni Kama Kupiga "Hatua Mbele"

The Blues wameshinda mechi mbili pekee kati ya saba zilizopita chini ya Potter, ambaye alichukua nafasi ya Thomas Tuchel mnamo Septemba, huku kukiwa na matokeo mabaya ambayo hayaridhishi.

Potter alifanya mabadiliko saba kwenye kikosi chake cha kwanza kutoka kwa kikosi kilichofungwa 1-0 na Arsenal kwenye Ligi ya Primia Jumapili lakini kocha huyo bado ana kazi ya kufanya klabuni hapo.

Potter aliwaambia waandishi wa habari. “Ni wazi, tumesikitishwa na matokeo lakini kwa jinsi tulivyocheza, tulitengeneza nafasi nzuri, kulikuwa na muundo bora na kiwango cha utendaji.”

Potter : Kupoteza Dhidi ya City ni Kama Kupiga "Hatua Mbele"

Vijana wa Potter watakwenda kumenyana na Newcastle United walio katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi kuu ya Uingereza Jumamosi katika mchezo wao wa mwisho kabla ya mapumziko ya Kombe la Dunia, huku  Chelsea wakiwa  hawajashinda katika mechi nne za ligi.

Kocha huyo alisema kuwa wana wasiwasi ambavyo hawapati matokeo wanayoyataka, uchezaji wao haujawa vile ambavyo wanavyotaka katika michezo iliyopita. Mchezo mkubwa unafuata mbele yao dhidi ya Newcastle huku wakiwa wanacheza vizuri, lakini lazima tutapambana kupata pointi 3.

Potter : Kupoteza Dhidi ya City ni Kama Kupiga "Hatua Mbele"

Potter alifurahishwa na kiungo wa kati Lewis Hall mwenye umri wa miaka 18, baada ya mchezaji huyo wa Kimataifa wa Uingereza kupata mwanzo wake wa pili wa maisha kwa The Blues, mchezaji huyo  alicheza dakika 75 na alipata nafasi nzuri iliyookolewa na kipa wa City Stefan Ortega.


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa