Christianinho mtoto wa Christiano Ronaldo alimsikia baba yake akisema “Kaka kwenye umri kama wa Mwanangu mimi nilikuwa na njaa kali ya mafanikio, sikuwa na uhakika wa kula hivyo kila siku uwanjani ilikuwa vita ya mafanikio kwangu”

Yalikuwa ni maneno ya Cristiano Ronaldo akiongea na rafiki yake Khabib bingwa wa UFC, Ronaldo akiamini kuwa huenda Mwanae asiwe na njaa kama yake kwakuwa tayari ana kila kitu
Ronaldo kuna muda alilazimika kusafiri na Familia yake Mpaka Ureno, kisiwani kwao Funchal Madeira kwenye mtaa wake wa asili wa San Antonio, yote hii ni kumpa hasira Mwanae, ajue maana ya Maisha
Mtoto wake alipewa Rafiki yake Miguel Paixao waliokuwa Wana tangu zamani kisha Mkewe Georgina alikuwa na Kaka wa Ronaldo anaitwa Hugo, walizungushwa kila Mtaa na kila hatua Ronaldo alipitia mpaka alipo leo, machozi nusu yawatoke
Eneo la San Antonio ni Kaskazini Mashariki mwa kisiwa cha Madeira, kuna majengo marefu ya zamani, hapo kuna mchanganyiko wa Wazungu na watu weusi ndio Ronaldo alikuwa anaupiga mpira eneo hatarishi sana, Mwanae aliumia sana kuona palivyo
Ronaldo anamjenga kisaikolojia Mwanae na Mkewe ili Mtoto apambane na Mkewe apambane kuwasimamia watoto, ndio maana amekuwa akihudhuria mechi karibia zote za Watoto Juventus
Cristiano Jr akirejea nyumbani hali vyakula laini, bali ni diet maalum inayosimamiwa na Daktari wa Baba yake, inaaminika wameanza kumjenga kifiziki kuenda na mikiki ya soka, ndio maana kwenye umri wake yupo fit sana
Cristiano Jr ama Christianinho akitoka mazoezini au kwenye mechi anaingizwa kwenye barafu, maumivu yake yanatibiwa kwa barafu na kuanza kumjenga misuli ingali mdogo, kitaalamu wanalimit Inflammatory reaction
Baba yake anaishi hivyo ndio maana sio injury prone, barafu inasaidia sana japo huku kwetu Mtu anaaza nayo ukubwani, ukimtazama Cristianinho unaweza kuhisi ana bata sana ila anapitia matayarisho makubwa kuvaa viatu vya Baba
Mama yake Georgina ni Mtalaam wa mazoezi pia, familia ina Physio wao pia, si ajabu siku moja baridi na mvua pale Lisbon, ila Ronaldo akaenda na Mwanae uwanjani akimfundisha target na kupiga kwa nguvu, sio ajabu alikuwa anafanya nae mazoezi mazito kipindi cha Karantini
MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Dogo akifata nyayo za baba itakuwa njema